4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Year > 2013
Results: 22 to 22 of 22
  • Zanzibar Unyago

    Country  Zanzibar
    Genres roots traditional
    FestivalSauti za Busara 2013
    Zanzibar Unyago
    Zanzibar Unyago

    Unyago ni ngoma ya kimila ambayo hupigwa na wanawake kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wasichana ambao wameshafikia umri wa kuolewa ili waweze kulinda ndoa zao na waume zao, na haya ni matayarisho kabla ya ndoa.

    Unyago ni ngoma maarufu katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki, kwa miaka mingi sasa ngoma ya unyago ilikuwa inapigwa na Kidude bint Baraka al maarufu Bi Kidude, ambaye kwa sasa anakadiriwa kuwa miaka zaidi karne, ametakiwa kuacha kuimba kutokana na hali yake kiafya sio nzuri. Kikundi cha Unyago kinaendelea na maonyesho na ni walewale waliokuwa na Bi Kidude wakifanya maonyesho ndani na nje ya nchi kama Japan, Poland, Afrika Kusini, Msumbiji, Ufaransa, Uholanzi na Ujerumani.

    Mpiga ngoma ya msondo Saada Ally Shoka maarufu Binti Ally wakishirikiana na Fatma Hamza na Bi Nachum Ngwali Faki wanaendelea kupiga ngoma huku Fatma Juma kwa sasa anaimba na kucheza. Usikose kuona onyesho lao ndani ya jukwaa la tamasha la sauti za Busara 2013 ikiwa ni mara yao ya kwanza kuonekana bila ya kiongozi wa Bi Kidude.