Results: 25 to 25 of 60
Shamsi Music
Country Kenya Genres band traditional jazz fusion Website www.shamsi.co.ke Facebook /ShamsiMusicKenya Festival Sauti za Busara 2019 Recordings 📼 The Audition, 2017; AfroSynthesis, 2019
Shamsi Music ni bendi inayopiga Afro-Jazz kutoka Nairobi, ambayo inajinasibu katika kutunga nyimbo zinazogusa mioyo na akili za watu. Mwanzo wa safari yao kimuziki walifikiria kutunga nyimbo zenye kuangazia sauti za Kenya na Afrika kwa ujumla.
Sauti yao inaweza kuelezewa kama ni jazz ya watu wa Kenya iliyoingizwa na mashairi imara.
Shamsi Music ilianzishwa rasmi mwaka 2014 chini ya uongozi wa Paul Mbithi na Laka Waithaka, baada ya kufanya onyesho pamoja. Miaka miwili baadaye, walichaguliwa kuingia kwenye tamasha la Safaricom International Jazz na kuwa ni bendi change pekee, tamasha liliwakutanisha wasanii nguli kama Fatoumata Diawara, Roberto Fonseca, David Sanborn na Manu Dibango. Watu wakaanza kupenda muziki wao, na wakashinda tuzo ya Café Ngoma kama kikundi cha Jazz Bora 2017.
Mwaka 2018, walifanya onyesho kwenye tamasha la Jazzy Koum Ben mjini Bamako, Mali, na DoaDoa nchini Uganda.
With thanks to Africalia