4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Year > 2015
Results: 25 to 25 of 36
 • Mwahiyerani

  Country  Tanzania
  Genres traditional
  FestivalSauti za Busara: 2015

  Mwahiyerani Group @ MaKuYa Festival 2013 - trailer

  Mwahiyerani
  Mwahiyerani

  Mwahiyerani ni kikundi cha ngoma za asili kutoka kijiji cha Mchauru Juu, Mkoani Mtwara. Aina yao ya kabila la waMakua ambao wanapatikana Kusini mwa Tanzania na Kaskazini mwa Msumbiji. Aina ya ngoma yao ilikua ikichezwa na watu wazima tu katika sehemu zilizojificha kuanzia miaka ya 1920. Kwa sasa inachezwa wazi na wanachama wa kundi hilo ni vijana wadogo wanaume kati ya umri wa 5 – 40. Kikawaida, kundi hilo hutumbuiza katika sherehe za kimila zikiwemo jando na unyago. Mwahiyerani ina wanachama hai 30 lakini kwa maonesho ya ‘mbali’ hua wanapunguza washiriki hadi 15 ambao 5 kati yao watakua waimbaji na wapiga ngoma. Nyimbo zao nyingi ni za kusherehekea vitendo vya kijasiri na ibada nyingine za asili.