Results: 4 to 4 of 4
Roland Tchakounté
Country Cameroon France Genres jazz blues Website www.roland-tchakounte.com Festival Sauti za Busara 2017 Recordings 📼 Abango, 2005; Waka, 2008; Blues Menessen, 2010; Ndoni, 2012; Ngueme and Smiling Blues, 2016
RolandTchakounté alizaaliwa Cameroon na kwanza alianza kujifunza kupiga ngoma, ikisha akajifunza kupiga guitar, akapiga kinanda na pia harmonica. Muziki wake ni mseto wa muziki wa blues na mziki wa asili ya kiafrika na anaimba kwa lugha ya Bamiléké ambayo ni lugha ya kabila lake.
Kupitia muziki wake, Tchakounté anaongelea kuhusu ukandamizaji unaofanyika dunianai na jinsi bara la Afrika linavyodidimia kimaendeleo, na kwamba kila habari inayotoka barani humu ni ya kusikitisha.
RolandTchakounté anapenda muziki unaopigwa na Elmore James na pia Muddy Waters lakini anafurahia na kupenda zaidi muziki wa John Lee Hooker na Ali Farka Taore ambao kwake ni wakufunzi wa muziki wa blues.
Tchakounté ametembelea na kupiga muziki nchi nyingi zikiwemo Ubelgiji, Canada, Indonesia, Vietnam, Malaysia, Lithuania na Croatia. Pia amepiga muziki nchi nyingi za kiafrika na Ufaransa. Ametoa albamu tofauti,na albamu yake ya “Ngueme and Smiling Blues” ndio inatamba sasa.
with thanks to Spedidam