4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: By Country > Madagascar
Results: 4 to 4 of 4
  • Tsiliva

    Country  Madagascar
    Genres roots traditional
    Website /pages/TSILIVA/134125855260
    FestivalSauti za Busara 2015
    Recordings📼

    Oh ! Le Tsiliva (2004); I Love You (2007); Sorry (2010); Mikisakisaky (2013)

    [Tsiliva] EPK 2014

    Tsiliva
    Tsiliva

    Jina la kuzaliwa la Tsiliva ni Tsiliva Diddiot, ni mwanamuziki waki malagasi ambaye huimba Kilalaka, aina ya muziki wakitamaduni kutoka kusini-magharibi ndani ndani nchini Madagascar. Akiwa mtoto wa mchungaji alizaliwa mwaka 1982 na kulelewa Kusini katika pwani ya mji Ambovombe Androy, karibu na Morondava. Akiwa mtoto, alipendelea kupiga muziki na kuandika nyimbo. Alipofika shule ya sekondari, aliunda au kujiunga na vikundi vingi ambavyo alitumbuiza navyo na kuandika muziki vikiwemo Cabalero Music, Tsirangoty, Diddiot Pro, Calypso, Mentalis Music na Foud Music. Baada ya kumaliza shule ya sekondari na kujipatia baccalaureat katika Usimamizi na mawasiliano, alianza kupiga besi katika kundi la Dadah de Fort Dauphin, baadae alijiunga na makundi Terana na Terakaly kama mpiga ngoma. Akiwa na Terakaly, alitumbuiza kwa mara ya kwanza katika tamasha kubwa, Donia music festival huko Nosy Be.


    Alianza kazi ya muziki binafsi mwaka 2004 na nyimbo yake ya kwanza iliyompa umaarufu Oh! le Tsiliva, iliyotoka Disemba mwaka huo, ilimpa mafanikio. Tamasha lake la kwanza kama Tsiliva lilikua mwaka 2005. Tangu alipotoa albamu mbili, CD za video 3 na nyimbo pamoja na Vaiavy Chila iliyoitwa Chilalaky, ambavyo vyote vilikua na mafanikio katika pande zote katika kisiwa. Huendelea kufanya ziara katika eneo lote la Madagascar na visiwa vya Bahari ya Hindi akifanya angalau shoo mbili kwa wiki, na mara nyingi akitumbuiza kwa ajili ya wamalagasy wanaoishi nje ya nchi huko Ufaransa. Kwa kawaida hutumbuiza na kundi kubwa la wanamuziki wakiwemo waimbaji sita, waimbaji wasaidizi watano pamoja na madensa.
     


    Lengo la Tsiliva ni kufanikisha upatikanaji wa muziki wa kimalagasy duniani kote. Anaweza kupiga Ngoma, gitaa na kucheza. Ingawa mara nyingi hutumbuiza kilalaka, mara kadhaa pia huchanganya aina nyingine za muziki ikiwemo pop na raga. Ukiacha utumbuizaji wake wa muziki, yeye pia ni injinia wa sauti kwa bendi nyingine.
     

    LMR-final-1-01
    with support from Libertalia-Music Records