4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: A - Z > S
Results: 32 to 32 of 60
  • Simba & Milton Gulli

    Country  Mozambique
    Genres hiphop
    Website /simbamiltongulli
    FestivalSauti za Busara 2017
    Recordings📼

    "The Heroes - A Tribute to A Tribe Called Quest", 2013

    Simba & Milton Gulli Kick It Chuta

    Simba & Milton Gulli
    Simba & Milton Gulli

    Simba alianza kuupenda muziki wa hiphop kwenye miaka ya 1990 alipokuwa akisikiliza rikodi za vikundi vya hiphop kutoka marekani kama vile De La Soul, Common na Tribe Called Quest.  Akaanza  kuimba muziki wa rap akiwa ana umri wa miaka 13.  Kuanzia hapo tena hakusita, aliendelea kwenye sanaa hii ya muziki na kuundeleza muziki huo nchini Mozambique.

    Simba alipewa jina la Nelson Angelo Sitoi na wazazi wake. Albamu yake ya mwanzo ya mtindo wa hiphop iliitwa Run and Tell your Mother na kwa wakati huo alipata nafasi ya kuwa msanii pekee wa hiphop kufanya maonyesho kwenye tamasha la Jazz huko Mozambique.

    Pia ni muanzilishi wa kikundi cha Simba na Rocats, ambacho ni kikundi kinachopiga live hiphop.  Simba alipiga kwenye tamasha la Busara la mwaka 2010 na alishabikiwa kiasi cha kwamba shoo yake inaongelewa hadi leo.

    Milton Gulli ni mwanamuziki na Prodyuza mwenye sifa za umahiri huko Mozambique.  Alianza muziki akiwa na kikundi kiitwacho ‘Philharmonic Weed’.  Amerikodi na kufanya maonyesho katika nchi tofauti duniani, ikiwemo Panama na Ureno, na ni mpigaji wa aina tofauti za miziki kama jazz, funk, soul na hiphop.

    Hivi karibuni, Simba na Milton Gulli waliachia albamu yao ya The Heroes – A tribute to A Tribe Called Quest iliyorikodiwa live nchini Mozambique.  Albamu hii ni ya kuwashukuru kikundi hichi cha hiphop cha A Tribe Called Quest, ambacho ndicho kilikuwa mingoni mwa vikundi vya mwanzo vya hiphop nchini Marekani.  Wao walikuwa hawana woga kwenye utunzi wa mashairi yao yenye ujumbe wa masuala ya kijamii na pia walisafisha njia ili vikundi vilivyokuja kufuata nyayo zao bila ya woga.

    Muziki wa Simba na Milton Gulli utawasha moto jukwaani, usikose kuwaona.

     

    travel sponsor Simba & Milton
    with thanks to Pro Helvetia