4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Genre > hiphop
Results: 36 to 36 of 50
  • Rico & the Band

    Country  Zanzibar
    Genres fusion hiphop
    Website /public/Rico-Single
    FestivalSauti za Busara 2015, 2017
    Recordings📼

    Champagne, 2010; Amani ndio Furaha Yetu, 2015

    RICO SINGLE-MADEMU WAZURI OFFICIAL VIDEO from ZANZIBAR TANZANIA

    Rico & the Band
    Rico & the Band

    Rashid Amin Abdallah kwa jina jengine, Rico Single ni mzaliwa wa kijiji cha Kikuu, Pemba. Rico Single alianza harakati za mziki akiwa shule ya msingi Kigamboni jijini Dar es Salaam alipokuwa anaishi na baba yake, alijiunga na kikundi cha Ngoma cha shule ambacho kilikuwa kinapiga Ngoma mbalimbali za asili kama mdundiko, chakacha na nyinginezo. 

    Kuanzia hapo akapata msukumo wa kuipenda sanaa, mwaka 2001 alikuwa mmoja wa waanzilishi wa kikundi cha sanaa ya maigizo walichokipa jina “Swahili Arts Group” ambacho kilikuwa na vijana wengi wenye vipaji mbalimbali. Kundi liliendelea na sanaa mbalimbali kama maigizo, sarakasi na mziki wa kizazi kipya, zenji flava.

    Mwaka 2004 walipata nafasi ya kushiriki kwenye tamasha la Bagamoyo (TaSUBa) na kupata nafasi ya kushiriki kwenye semina.

    Mwaka 2005 walielekeza nguvu zao kwenye sanaa ya mziki, na walifanikiwa kutoa nyimbo yao ya kwanza waliyoipa jina “Hii Sanaa” na “Fadhila za Punda” waliyoirekodi kwenye studio ya Baucha. Kundi la Swahili Arts Group lilisambaratika mwishoni mwa mwaka 2005, kipindi cha kukaribia uchaguzi ambapo wasanii wengi walichukuliwa kufanya kazi mbalimbali.

    Baada ya kundi la Swahili Arts Group kusambaratika Rico Single aliamua kusimama peke yake na kuelekeza nguvu kwenye mziki wa kizazi kipya, Zenji Flava.

    Mwaka 2006 alifanikiwa kuingia studio za “Heart Beat Records” chini ya mtaarishaji Hababuu mwana Zanzibar akatoka na kibao “Hili Game” hatimaye kibao kilipokelewa vizuri na kumpa hamasa zaidi ya kuendelea na kazi. Mwaka huo huo,kwa mara ya kwanza zilianzishwa tuzo za muziki Zanzibar (Zanzibar Music Award) nyimbo yao waliyowahikuitoa kipindi cha Swahili Arts Group “Fadhila za Punda ilipata tuzo.

    Mwaka 2007 alitoa nyimbo nyingine akimshirikisha Berry Black, Shirko na Small X aliyoipa jina la “Yaache Mambo ya Klabu” ndani ya Teddy Records ikisimamiwa na Shirko, kwa bahati mbaya nyimbo ilivuja.

    Mwaka 2008 alitoa nyimbo nyingine aliyoipa jina la “Nitampataje” akishirikiana na Kassim Mganga na baadae kidogo akatoka na nyingine akishirikiana na Sultan King akaipa jina “Tuongee kidogo” na mwaka huohuo akapata nafasi ya kushiriki kwenye tamasha la Kimataifa la Filamu (ZIFF)

    Mwaka 2009 akatoa nyimbo nyingine akishirikiana na Baby Jay “Wacha waongee” ikiwa imefanya vizuri mpaka mwaka 2010 ambapo akashirikiana na AY na kibao “Shampen”