4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Most Popular
Results: 369 to 369 of 441
  • Ze Spirits Band

    Country  Tanzania
    Genres band fusion
    Website /Ze-spirits-band-456702374465159
    FestivalSauti za Busara 2017
    Recordings📼

    Safari, 2014; Mwizi, 2014

    ze spirits band - moto

    Ze Spirits Band
    Ze Spirits Band

    Ze Spirits Band ni kikundi cha wanamuziki mahiri ambao walianza pamoja tokea wakiwa wadogo,walipokuwa wana miaka saba hadi kumi tu.  Sasa wanamuziki hawa wanaumri wa miaka 18 na kwenda juu. Walianza muziki umri huo mdogo chini ya ulezi wa Vitali Maembe huko Chuo Cha Sanaa cha Bagamoyo.

    Muziki wao unatokana na ngoma za jadi na asili japokuwa wanaimba nyimbo mpya na wanachanganya na muziki wa kizazi kipya.  Wanapokuwa jukwaani wao huwafurahisha na kuwachangamsha watazamaji wao. 

    Kikundi hichi kina wasanii sita kwa sasa na wameshiriki kwenye matamasha mengi hapa Tanzania kama vile tamasha la Bagamoyo, Tamasha la Beat, Tamasha la Karibu, na pia kufanya maonyesho yao hapo Alliance Francaise na Chap Chap Event hapo Dar es Salaam.