4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Most Popular
Results: 375 to 375 of 441
  • Mcharuko Band

    Country  Zanzibar
    Genres band pop fusion
    Website www.zanzibarmusic.org
    FestivalSauti za Busara 2017
    Mcharuko Band
    Mcharuko Band

    Kikundi hichi cha Mcharuko kimeundwa mwaka 2015 na wasanii watano waliobobea kwenye sanaa hii ya muziki, wasanii hawa ni wanafunzi kutoka chuo cha muziki Zanzibar (Dhow Countries Music Academy).

    Bendi iliundwa kwa madhumuni ya kufanya maonyesho ya kila wiki kwenye bustani za Forodhani au hata kwenye maeneo mengine ambayo wataruhusika kupiga muziki bila ya kiingilio.  Madhumuni makubwa ni kuwasogezea wananchi sanaa ya muziki asilia.

    Mcharuko kama jina linavyomaanisha, wanapokuwa jukwaani hucharukwa na kutumbuiza kwa ushabiki mkubwa.  Vijana hawa piawanapiga aina tofauti za muziki kama vile jazz, fusion, afro jazz na taarab.