4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Most Popular
Results: 383 to 383 of 441
  • The Nile Project

    Country  Nile Basin
    Genres acoustic fusion roots
    Website www.nileproject.org
    FestivalSauti za Busara 2014
    Recordings📼

    Aswan, 2013 (https://soundcloud.com/nileproject)

    The Nile Project
    The Nile Project

    Ni Historia ya Mto Nile huwaunganisha watu kitamaduni na kimazingira. Hutengeneza mfumo wa kimazingira kati ya Misri, Tanzania, Uganda, Kenya na Ethiopia. Huwakutanisha wanamuziki kutoka Burundi, Kongo, Misri, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan ya Kusini, Sudan, Tanzania na Uganda, Mradi huu wa Nile huwaunganisha na kuwa sauti moja.
     
    Mkusanyiko wa kwanza ulikutana mjini Aswan, nchini Misri kwa muda wa wiki mbili, mwezi Januari mwaka 2013, Nyimbo mpya zilitungwa zenye vionjo za ala mbalimbali za asili. Huo ndio ukawa mwanzo wa albam ya kwanza iliyorekodiwa moja kwa moja. Mkusanyiko wa waimbaji 6 na lugha 11 tofauti. Nyimbo zenye kuhamasisha umoja na mahusiano ya ndani na nje ya nchi wanazotoka.

    Muungano ambao ulizaa umoja wa tamaduni mbalimbali ambazo walizozizoea na kuziunganisha. Katika mjumuiko huo uliokutana Aswan, ulihudhuriwa na Masenkop ‘Sudan’, Simsimiya na Tamboura ‘Misri’ na baadae kukutanisha Masenko ‘Ethiopia’ na Endingidi ‘Uganda’. Waandaaji Mina Girgis na Mile Jay walitaka kuonyesha mchanganyiko wa ala za asili zilizowazunguka kama Saksafoni ya Ethiopia na Kwa upande wa Misri Ney, Oud na Violin, pamoja na Gitaa.