4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Recently Clicked
Results: 395 to 395 of 441
  • Atse Tewodros Project

    Country  Ethiopia Italy
    Genres jazz traditional
    Website www.atsetewodros.org
    Facebook /EthioItalianband
    FestivalSauti za Busara 2023
    Recordings📼Maqeda, 2022

    Atse Tewodros Project "Set Nat" (Official video)

    Atse Tewodros Project
    Atse Tewodros Project

    Atse Tewodros,Ni mradi unaoratibiwa na mwandishi-mwanamuziki-mwimbaji wa Ethio-Kiitaliano Gabriella Ghermandi, kwa lengo la kuanzisha ushirikiano kati ya wanamuziki wa kitamaduni wa Ethiopia na Italia. Ni mradi unajumuisha nyimbo kutoka kwa Upinzani wa Ethiopia ambao ulipigana dhidi ya Utawala wa Kifashisti wa Italia. Kwa kufanya hivyo, inarejesha yaliyopita, inaelezea mwenendo wa maisha ya binadamu na wahamiaji na kuunda njia za kujadili utambulisho.

    Kundi kamili linaundwa na wanamuziki 9:

    Gabriella Ghermandi - sauti, Fabrizio Puglisi – piano, Misale Legesse – Seti ya ngoma ya kitamaduni ya Ethiopia, Endris Hassen –upinde wa kamba moja "Masinko", Camilla Missio - gitaa la besi, Abu Gebre – mwanaethiopia filimbi ya kitamaduni "Washint", Tommy Ruggero - ngoma, Anteneh Teklemariam - acoustic na krar ya umeme (Ethiopian lyre), Misikir Mindaye Tawi - sauti na sauti za kuunga mkono.

    Gabriella Ghermandi, kiongozi wa kikundi hicho anasema “Nilikulia katika ulimwengu uliojaa sauti tofauti: Waethiopia, Waitaliano, Wakongo, Wahindi. Mama yangu alisimamia duka la nguo huko Addis Ababa, katika barabara kuu ya mtaa wa Piassa. Karibu naye kulikuwa na duka la muziki lililoendeshwa na mwanamke wa Kigiriki, ambaye aliuza vyombo, wachezaji wa rekodi, rekodi za 33 na 45 rpm. Katika duka lake nilisikiliza muziki wa Beatles, Zorba na Rebetika wa Kigiriki. Nikiwa narudi nyumbani nilikuwa nasikiliza muziki wa waimbaji wetu wa Azmari. Hatimaye nilipofika nyumbani redio ilikuwa inawashwa wakati baba yangu hayupo kwani hakufurahia wala kupenda muziki wa Ethiopia Alikuwa akiielezea kuwa ni kama kuomboleza,lakini mimi na rafiki zangu tuliupenda.

    Nilisikiliza waimbaji wa Italia; muziki ambao wanafunzi wenzangu wa Italia waliupenda. Pia nilisikiliza muziki wa Kikongo wa rafiki yetu Geraldine, muziki wa Kihindi wa majirani zangu wa Kashmiri, bila shaka Bob Marley, pia bendi ya muziki ya rock ya Uingereza Genesis.

    Hatimaye, kulikuwa na nyimbo za vita. Sikuwapenda siku hizo. Nilikuwa nikienda na binamu zangu kuona gwaride la kusherehekea ukumbusho wa ushindi wetu huko Adwa na kukombolewa kutoka kwa utawala wa Kifashisti, ili tu kucheka ishara za wapiganaji wanaoimba nyimbo hizo za vita. Walipofumbua macho yao sana, wakitoa panga na ngao zao, walipiga kelele za vitisho kwa adui zao. Nilikuwa nikiwaona kichekesho. Enzi hizo, ningemwona mtu yeyote kuwa ni kichaa ambaye aliniambia kuwa siku moja nitawakumbuka kwa kuiga mienendo yao kwenye jukwaa la sinema ulimwenguni kuwakumbuka wazee wetu waliopigania uhuru.

    Muziki hutoa sauti kwa sauti ambazo hazijaonyeshwa. Muziki haumaanishi siasa bali unaingia kwenye siasa, katika kujenga jamii, katika maisha ya mtu. Muziki ni njia ya kutoa maono ya wakati ujao unaowezekana au usiowezekana."

    Atse-Tewodros-Project-Travel-Sponsor
    With thanks to Culture D'europa - Regione Emilia Romagna https://culturaestero.regione.emilia-romagna.it/it & Italian Embassy in Dar-es-Salaam, Tanzania https://ambdaressalaam.esteri.it/ambasciata_daressalaam/it