4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: By Country > Germany
Results: 4 to 4 of 4
  • Pat Thomas & Kwashibu Area Band

    Country  Ghana Germany
    Genres afrobeat band roots
    Website www.strut-records.com
    FestivalSauti za Busara 2017
    Recordings📼

    : Pat Thomas and Kwashibu Area Band, 2015

    PAT THOMAS & KWASHIBU AREA BAND, Live in Berlin, October 20, 2015

    Pat Thomas & Kwashibu Area Band
    Pat Thomas & Kwashibu Area Band

    Pat Thomas ni muimbaji anaetokea Ghana na ni mashuhuri kwa uimbaji wake wa aina ya muziki iitwayo ‘highlife’ kutokea huko Ghana. Alikuwa ni mmoja wa waimbaji kwenye kikundi cha Ebo Taylor.  Pia anapiga aina tofauti za muziki ikiwemo Afrobeat and Afro-pop.

    Alizaliwa Agona huko jimbo la watu wa Ashanti nchini Ghana.  Yeye tangu azaliwe amezungukwa na muziki.  Baba yake ni mwalimu wa muziki na mama yake ni muimbaji kwenye kikundi cha ngoma.  Mjomba wake ni King Onyina ambaye ni mpigaji guitar maarufu sana nchini Ghana.  Pat Thomas aliishi na mjomba wake huyo na kujifundisha kusoma alama za muziki, baadae alijifundisha kupiga guitar na ngoma.  Akakulia kuwa mtungaji na mwandishi mzuri wa muziki, na kuanza kuimba kwenye vilabu vya starehe.

    Kwenye miaka ya 1970, alihamia Accra na kujiunga na kikundi cha Ebo Taylor ambacho kilikuwa ni kikundi kinachoheshimika na kupendwa na washabiki kwa kupiga aina tofauti za muziki kama Afrobeats, Afro-Latin, Reggae na African Disco.

    Mwaka 1982 alihamia uingereza na kurikodi kwenye studio za Hitsville akiwa na Ebo Taylor na Uhuru Yenzu.  Kibao chake cha mwanzo ambacho kilimpatia umaarufu huko ulaya kinaitwa Asanteman hapo mwaka 1985. Baada ya hapo alifanya ziara za nchi tofauti barani ulaya, ziara hiyo iliendeea kwa muda wa miaka mitano mfululizo na kurikodi albamu tofauti.

    Alihamia Canada mwaka 1990 na akawa anafundisha kwenye chuo kikuu huku akiendelea kupiga mziki na kufanya rekodi.  Akatoa albamu yake mwaka 1991 na kushinda albamu bora ya mwaka.  Baada ya rekodi hii, alikuwa akifundisha tu kwa kipindi kinachokaribia  miaka kumi.

    Mwaka 2015, studio za Strut zilitoa rekodi yake ya mwanzo iitwayo Pat Thom as and Kwashibu Area Band, iliyorikodiwa huko Accra.  Wakati akirikodi alifanya kazi na wasanii mashahuri  kama Kwame Yeboah na Ben Abarbanel-Wolff pia na wasanii chipukizi kama Tony Allen, Ralph Karikari na hata mwanawe mwanamke ambae ni muimbaji anaeitwa Nanaaya.

     

    travel-Embassy-of-the-Federal-Republic-of-Germany
    with thanks to Embassy of Germany