4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Genre > hiphop
Results: 47 to 47 of 50
  • Wakazi

    Country  Tanzania
    Genres jazz bongo flava hiphop jazz
    Website www.musicinafrica.net
    Facebook /wakazimusic
    Instagram /wakazi
    FestivalSauti za Busara 2020, 2024
    Recordings📼Abacus, 2014; Kisimani, 2018; Sauti za Busara 2020 (Live Album), 2021; Beberu: Reflections, 2023; Beberu: Declaration, 2023; Beberu: Affirmation, 2024

    Wakazi (Live Performance)

    Wakazi
    Wakazi

    Kutoka Tanzania, Wakazi (Webiro Wassira) alihamia Marekani kwa ajili ya kutekeleza azimio la Ndoto yake, lakini mapenzi yake kwa muziki yalimfanya abadili muelekeo na malengo yake.

    Akiwa amejitolea kusimamia ndoto yake na malengo kwa ustadi wa hali ya juu, kwa sasa akiwa nchini Tanzania, Wakazi anaonekana kuwa Balozi wa Hip Hop nchini Tanzania, akiwa na mtazamo wa kipekee unaotokana na historia yake tofauti na uwezo uliojengeka katika misingi ya utofauti wa kitamaduni aliojifunza katika nchi alizopata fursa kuishi.

    Anapenda n ani mahiri katika masuala ya kiufundi katika muziki, ana mvuto wa kibiashara, na ana uwezo wa kushughulikia masuala ya kijamii na kisiasa.

    Utofauti waka na umahiri katika tungo zenye mchanganyiko wa mashairi ya Kiingereza na Kiswahili ilimpa jina la “Bilingual Beast”.

    Uwezo wake wa kuunda muktadha kwa matumizi ya busara ya sitiari na uchezaji wa maneno ni wa kipekee na usio na mlinganisho, ukionyesha uzoefu wake wa maisha ya kibinafsi na akili yake ya kutafakari.