4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Genre > rumba
Results: 7 to 7 of 14
 • FM Academia

  Country  Tanzania
  Genres band dance rumba
  Website www.fmacademia.com
  FestivalSauti za Busara 2012
  Recordings

  Internet (1997); Atomic (1998); Prison (2000); Freedom (2001); Wapambe Nuksi (2002); Dunia Kigeugeu (2006); Vuta Nikuvute (2010)

  FM Academia
  FM Academia

  Jina lao la umaaarufu wanatambulika kama Wazee wa Ngwasuma ni moja kati ya bendi inayoongoza kwa kupendwa nchini Tanzania. Ni wataalamu wa muziki wa dansi ambao wamefanikiwa kuwateka mashabiki wa Tanzania hasa kwa aina yao ya uimbaji na uchezaji.

  Kundi hili lilianzishwa mwaka 1997 kwa jina la FM International, ambalo kwa sasa linafahamika kama FM Academia chenye kikosi kazi cha wanamuziki kutoka Tanzania na Congo (DRC). Hutumia vipaji na jitihada zao ili kuwaridhisha wapenzi na mashabiki wao wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla pale wafanyapo maonyesho yao.

  Walifanikiwa kutoa albamu yao ya kwanza mwaka 1997 waliyoipa jina la “Internet” ikifuatiwa albamu nyingine mwaka uliofuata 1998 iliyokwenda kwa jina la “Atomic”. Mwaka 2000 walifanikiwa kutoa albam yao kali ya tatu waliyoipa jina la “Prison” baada ya kutoka jela baadhi ya wanamuziki wao kutoka Congo ambao walikuwa wanashitakiwa kwa kosa la kukaa nchini bila ya vibali vya kuishi na kufanyia kazi. Baada ya hapo waliendelea kutoa albamu zao kali kwa kila moja kumshinda mwenzie na kufanikiwa kupata tuzo kutokana na kazi zao.

  Mara nyingi hufanya maonyesho ya kusisimua, onyesho lao katika tamasha la Sauti za Busara inategemewa kuwa kali zaidi ya hayo. Timu kamili ya wanamuziki 25 watapanda jukwaani siku ya mwisho ya kumalizia tamasha na kuhakikisha watakonga nyoyo za mashabiki wao wote watakaohudhuria siku hiyo. Tegemea onyesho kali zaidi kutoka kwa Wazee wa Ngwasuma, Wazee wa Mjini.