4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: A - Z > H
Results: 7 to 7 of 7
  • H_art the Band

    Country  Kenya
    Genres band
    Website www.penya-africa.com
    FestivalSauti za Busara 2017
    Recordings📼

    2004 Nikikutazama; 2015 Lovephobic

    H_ART THE BAND - NIKIKUTAZAMA (OFFICIAL VIDEO)

    H_art the Band
    H_art the Band

    H-Art the Band ni kikundi cha wasanii watatu Mordecai Kimeu, Kenneth Muya na Wachira Gatama.  Walikutana walipokuwa wakifanya mazoezi ya kuingia kwenye sanaa ya uigizaji mwaka 2012 huko kwenye jumba la Taifa la Sanaa ya Maigizo, Kenya.  Wakati wakifanya mazoezi walijikuta wote wanapenda muziki, mashairi, sanaa ya vichekecho, ngoma na hadi mtazamo wao wa kimaisha unafanana.  Hivyo wakakubaliana kuunda kikundi chao cha H-art the band, baada ya hapo wakajiunga na program ya Sauti Academy ambapo walihitimu mwaka 2014.

     

    Sanaa ya H-art the band ni mchanganyiko wa nyimbo nyororo, mashairi, rap, uigizaji, ngoma na pia mitindo ya mavazi.  Sanaa na muziki wa kikundi hichi inapendwa na watu wa rika zote.  Mordeci na Wachira wao ni washairi na waimbaji na Kenchez ni mpigaji kinanda cha guitar.

     

    Kwa kipindi cha mwaka uliopita, H-art the band walikuwa wakifanya maonyesho mfululizo, kila sehemu na hadi majiani.  Hivyo, hili limewajengea ukakamavu na umashuhuri kwenye jukwaa la muziki nchini Kenya.

     

    travel-Africalia
    with thanks to Africalia