4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Genre > rumba
Results: 9 to 9 of 14
 • Jupiter & Okwess International

  Country  DRC
  Genres band rumba urban
  Website jupiter-okwess-international.com
  FestivalSauti za Busara 2014
  Recordings

  Hotel Univers, 2013

  Jupiter & Okwess International BBC Africa Beats

  Jupiter & Okwess International
  Jupiter & Okwess International

  Jupiter Bokondji alizaliwa Kinshasa nchini Congo miaka 48 iliyopita kutoka katika familia ya wanamuziki. Bibi yake alijulikana sana kama mtabibu wa jadi, alitambulika kwenye muziki wa jadi kama Zebola kutoka Ekonda ngoma ambayo inasemekana inatibu magonjwa mbalimbali. Jupiter katika utoto wake alikuwa anaongozana na bibi yake kwenda kanisani na harusini kwa ajili ya kufanya maonyesho. Alitumia ujana wake mjini Berlin nchini ujerumani ambako baba yake alichaguliwa kuwa Afisa Ubalozi wa Kongo nchini Ujerumani mwaka 1974, ambapo aliweza kuijua Ulaya na wadau wa muziki kama the Stones, Deep Purple, James Brown na wengineo. Alianzisha kundi lake la muziki wa Rock lijulikanalo kama "Der Neger" na rafiki yake wa kijerumani, ulikuwa mchanganyiko wa Mongo (Ala ya asili) na Gitaa. Hatimaye bendi ikapata umaarufu maeneo yote ya mjini. Akiwa na umri wa miaka ya kati ya ishirini bendi ilipata safari ya kwenda Kongo ambako alipata fursa ya kutafuta sauti nyingine ambapo alifikiria kwamba sauti alizokuwa anazisikia Ulaya na zenye asili ya Kongo kutoka kwenye makabilia 450, na ambayo yamegawanyika kutokana na matatizo ya kisiasa yanaweza kuunganishwa pamoja. Aliendelea kubuni aina zake za kipekee akiwaunganisha wasanii wa barani ulaya. Mipango na mawazo yake ilikuwa kuirudisha miziki ya Kongo iliyokwisha anza kupotea. Alianzisha kundi la "Bongofolk" mwaka 1983 na kuliunda tena "Okwess International" mwaka 1990.