4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: A - Z > F
Results: 9 to 9 of 10
 • Fredy Massamba

  Country  Congo
  Genres funk hiphop roots urban
  Website www.traffixmusic.com
  FestivalSauti za Busara 2012
  Recordings

  Ethnophony (2010)

  FREDY MASSAMBA Album Ethnophony

  Fredy Massamba
  Fredy Massamba

  Muimbaji, mchezaji na mtumiaji wa chupa kama kifaa chake cha muziki si mwingine bali ni Freddy Masamba anarudi tena Zanzibar akiwa na kundi lake. Fredy mwenye asili ya Afrika ya kati anachanganya muziki wake wa soul, hiphop na funk. Akiendelea kufurahia kazi yake kwa miaka 11 ambapo alifanikiwa kufanya maonyesho na wasanii tofauti wakiwemo Zap Mama, Tambours de Brazza, Manou Gallo na Didier Awadi ambaye alipiga naye mwaka 2007 katika tamasha la Sauti za Busara.

  Alizaliwa Pointe-Noire, mji wa pili kwa ukubwa nchini Congo, Fredy aliendeleza kipaji chake kwa kuimba na kucheza. Mwaka 1998 Freddy alihamia Brussels kutokana na hali ya machafuko nchini Congo.

  Kama wanamuziki wengine ambao huamia ughaibuni, muziki wa Fredy unaonekana kama ni wenye mvuto na hisia kali katika harakati za mifarakano nchini mwake. Matokeo ya swala hili ni kwamba kufurahia, sauti ya mvuto ambapo hiphop si yenye kutengwa Afrika ya Kati.

  Alifanikiwa kutoa albamu yake ya kwanza ya Ethnophony ambayo iltengenezwa kwa muda wa miaka minne. Feddy alianza kurekodi kazi zake katika studio ya notorious Sankara iliypo Dakar, Senegal kitovu cha ubunifu wa hiphop za kiafrika. Hapo walikutana na Frédéric Hirschy ni mpiga gitaa la besi ambaye yupo naye kwa sasa, ambapo kwa pamoja walifanikiwa kutoa albamu.

  Mchakato huu ulianza taratibu kwa kuboresha uimbaji, mipango ilisimama kidogo alipokuwa na ziara ya kimuziki na Awadi na baadaye aliporudi alimalizia taratibu zote za muziki. Anaimba kuhusu nchi yake ambapo vita vya mwaka 1998 vilimfanya akimbie, matumaini yake ya baadae, fahari na ubunifu wa maisha ya watu wa Congo.

  Huimba kwa Kifaransa, Kikongo, Lingala au Kiswahili, awapo jukwaani hutumia kipaji chake kwa kuchanganya aina mbalimbali za vifaa vya muziki kama chapa ya soda hutumia kama filimbi. Hutumia uwezo wake wote akishirikiana na wenzake kama Yoann Julliard mpiga ngoma, Frédéric Hirschy mpiga besi na Jean Ferrarini katika kinanda na kufanya maonyesha ya kuvutia kabisa. Muziki wa upole wenye misingi ya hiphop, anajitahidi kuisukuma hiphop ya Afrika.

  logo Skinfama skyline
  With thanks to Skinfama