4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: A - Z > W
Results: 9 to 9 of 9
 • Wunmi

  Country  Nigeria UK USA
  Genres afrobeat dance
  Website www.wunmi.com
  FestivalSauti za Busara 2014
  Recordings

  African Living Abroad (A.L.A), 2007

  Wunmi
  Wunmi

  Wumni ni mzaliwa wa Uingereza aliyekulia nchini Nigeria na anafanya shughuli zake za kimuziki nchini Marekani, alirudi nchini Uingereza akiwa kijana kisha akahamia nchini Marekani. Kudumu kwa taswira ya Wunmi katika medani ya Muziki ilikuwa kipindi cha majira ya joto mwaka 1986. Rekodi yake ya kwanza aliwashirikisha wasanii pamoja na waandaaji wa Muziki kama Dennis Ferrer, King Britt, Jerome Snydenham, Osunlade, M.A.W., Bugz in the Attic, Ron Trent, Pasta Boys- na nyimbo yake ya kwanza alishirikiana na mkongwe Roy Ayres. Albamu yake ya kwanza aliyoipa jina "A.L.A- African Living Abroad" ilipongezwa na Gilles Peterson kuwa moja ya mafanikio katika safari yake ya muziki. Muonekano wa Wunmi awapo kwenye steji ulikuwa wa kuvutia na kumpatia umaarufu kutokana na bidii na ubunifu wake katika upangiliaji wa maonyesho yake. Aliwakonga mashabiki wake katika maonyesho mbalimbali kama Barbocon nchini Uingereza, Summer Stage nchini Japan na Big day nchini Australia. Nchini Nigeria alikuwa anaishi na mjomba wake gwiji la muziki Dr Victor Olaiyo ambaye alikuwa maarufu katika vituo vya redio na mitaa mbalimbali mjini Logos. Si tu Muziki bali Wunmi aliweza kutangaza kipaji chake kingine cha ubunifu wa mavazi ambapo aliporudi nchini Uingereza aliweza kuanzisha mitindo yake aliyoipa jina la Wow Wow.