ENG | FRE

Wito kwa Wasanii: Sauti za Busara 2021

 
CORONAVIRUS UPDATE

 

With regard to the global coronavirus (COVID-19) pandemic, we would like to assure everyone we are closely monitoring and assessing developments in order to make an informed decision on whether to proceed with the next edition of Sauti za Busara festival in Zanzibar during 11 – 14 February 2021.

We remain optimistic “the show will go on” and encourage all artists playing unique music connected to Africa to apply to participate. Our overriding priority is the safety and security of local Tanzanians, the broader music community and everyone involved in staging this high-profile event.

Keep safe and best wishes from Team Busara.

Sauti za Busara, ni moja kati ya matamasha makubwa zaid ya muziki barani Afrika, sasa liko katika maandalizi ya msimu wake wa 18. Litarindima tena huko Stone Town, Zanzibar tarehe 11 – 14 Februari 2021.
Wito kwa Wasanii utakuwa wazi hadi saa sita usiku (EAT) mnamo 31 Julai 2020.
Sauti za Busara huonyesha aina tofauti za muziki wa live na wa kiasili na uliochanganywa na wa kiasasa kutoka Bara la Afrika na diaspora. Wanamuziki wanaowakilisha Ulimwengu wa Arabuni na Bahari la Hindi pia wanakaribishwa kuomba.
Upendeleo utatolewa kwa:

 • Muziki wa kipekee utokanao na utamaduni wa Afrika, Ulimwengu wa Kiarabu na ukanda Bahari ya Hindi
 • Wasanii wanawake, au vikundi vinavyoongozwa na wanawake
 • Vijana, vipaji chipukizi.
 • Muziki wenye ujumbe mahsusi/mzuri, unaofaa na muhimu kwa jamii
 • Muziki ambao unafanywa ‘100% live’!
Music In AfricaLinki ya maelezo ya Music In Africa
Music In Africa (www.musicinafrica.net) ni jukwaa la taarifa na mabadilishano kwa wasanii kwa kiafrika. Ili kusaidia maombi yako tafadhali jisajili na Music in Africa hapo chini. Music In Africa inafanya kazi kama EPK (Electronic Press Kit) hivyo kama utaweka maudhui yenye mashiko kama maelezo ya Msanii, nyimbo zilizotoka hivi punde, za kuangalia na kusikiliza, itaongeza wigo wa uonekana na kupata mialiko ikiwemo Sauti za Busara na matamasha mengineyo.
Jisajili hapa kuweka maelezo yako kwenye Music in Africa

Ili Kuomba ushiriki, tafadhali tuma viambatanisho vyote vilivyoorodheshwa hapo chini. Maombi ambayo hayajakamilika au yaliyopokelewa baada ya tarehe ya mwisho hayatazingatiwa.

 • Fomu ya maombi*
 • Wasifu / Wasifu wa Wasanii *
 • Kama hujajisajili na Music In Africa, jisajili na ututumie link ya wasifu (profile) yako (http://www.musicinafrica.net)
 • Audio za hivi karibuni (tuma CD mbili kupitia posta, au nyimbo zisizidi 3 kwa WeTransfer / dropbox / google drive)
 • Video ya shoo za live (tuma DVD 1 kwa posta au clip1 kwa WeTransfer / dropbox / google drive)
 • Picha 2 kwa ajili ya matangazo (zenye ubora wa kuchapisha, 2MB kila moja)
 • Ramani ya jukwaa (Stage Plan) na mahitaji ya vifaa (Technical Rider) (ikiwa inapatikana)
 • Viambatanisho lazima viwe na lebo iliyo wazi na iwekwe kwenye (WeTransfer / dropbox / google drive) zitumwe kwa barua pepe journey@busara.or.tz

Maombi yaliyochapishwa yanapaswa kutumwa kwa anwani ifuatayo:
Journey Ramadhan
Meneja wa tamasha la Sauti za Busara,
Busara Promotions
P O Box 3635
Zanzibar
Tanzania

Tafadhali ainisha/andika kifurushi chako wazi wazi: “Contents not for sale. For promotional use only

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha fomu ya maombi ni saa sita usiku (EAT) tarehe 31 Julai 2020
Ikiwa umechaguliwa, Sauti za Busara itagharamia yafuatayo kwa wasanii wataoshiriki:

 • Malipo ya onyesho
 • Posho ya chakula
 • Malazi utakapokuwa Zanzibar
 • Usafiri wote wa ndani unaohusiana na shoo
 • Gharama za visa Tanzania
 • Pasi ya tamasha, zitakazokuwezesha kuhudhuria shoo zote wakati wa tamasha
 • Mwaliko wa Movers & Shakers (kongamano la wataalamu wa muziki), mikutano ya waandishi wa habari na hafla zingine
 • Wasifu (Profile) ya msanii katika programu za tamasha, vyombo vya habari, tovuti na majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Kamati ya uteuzi itakutana mnamo Agosti kwa ajili ya kuchagua na kutoa orodha ya Sauti za Busara 2021. Waombaji wataarifiwa kuhusu matokeo kabla ya Septemba.
Wasanii kutoka nje ya Afrika Mashariki kawaida wanahitajika kutafuta wadhamini wa usafiri watakaowawezesha kufika Zanzibar.