Wito kwa Wasanii: Sauti za Busara 2022

English Kiswahili Français

Wito kwa Wasanii: Sauti za Busara 2022

Sauti za Busara ni tamasha bora barani Afrika, sasa lipo kwenye maandalizi ya msimu wa 19. Kama kawaida tamasha lijalo litafanyika katika viunga vya Mji Mkongwe, Zanzibar kuanzia tarehe 11 – 13 February 2022.

Maombi ya wasanii yanapokelewa mpaka tarehe 31st July 2021.

Sauti za Busara huonyesha muziki mubashara jukwaani, halisi na anuai kutoka Bara zima la Afrika. Wanamuziki wanaowakilisha nchi za kiarabu na ukanda wa bahari ya hindi nao wanakaribishwa kufanya maombi ya ushiriki

Vipaumbele vitatolewa kwa:

 • Muziki wenye utambulisho wa kiafrika, Nchi za Kiarabu na Bahari ya Hindi
 • Wasanii wa kike, au vikundi vinavyoongozwa na wanawake.
 • Vijana, wasanii mpya na vipaji vinavyochipukia
 • Muziki wenye ujumbe unaogusa jamii
 • Muziki wenye kupigwa mubashara ‘LIVE100%’!

Ili ukamilishe maombi ya ushiriki, tafadhali tuma mahitaji yote yaliyoorodheshwa hapo chini. Maombi yasiyokamilika au yatakayochelewa hayatazingatiwa.

Link ya WeTransfer / Dropbox / Google Drive yenye viambatanisho/ mahitaji yote itumwe kwa journey@busara.or.tz  viambatanisho vitakavyotumwa lazima viandikwe (label) kiufasaha.

Mwisho wa kupokea maombi ya mahitaji yote ni usiku wa tarehe 31st July 2021

Ikichaguliwa, Sauti za Busara italipa gharama zifuatazo kwa wasanii wanaoshiriki(+ 1 mfanyikazi).

 • Malipo ya onyesho
 • Pesa ya kujikimu kwa ajili ya chakula na viburudisho
 • Malazi mtakapokuwa Zanzibar
 • Usafiri kwa ajili ya onyesho lako
 • Malipo ya visa, utafidiwa ikiwa utaleta risiti
 • Pasi za tamasha zima
 • Mualiko wa Movers & Shakers (kongamano linalokutanisha wataalamu wa Sanaa ya muziki), mkutano wa waandishi wa habari na matukio mengine
 • Wasifu wa msanii/ kikundi katika kitabu cha tamasha, taarifa za habari, tovuti na mitandao ya kijamii.

Jopo la uteuzi litakutana mwezi wa nane mwanzoni kukamilisha orodha ya wasanii kwa ajili ya Sauti za Busara 2022. Wasanii wote watajulishwa matokeo kabla ya mwezi wa tisa. Wasanii kutoka nje ya Afrika Mashariki wanatakiwa kutafuta wadhamini wa kuwasafirisha kuja na kuondoka Zanzibar.