4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: By Country > USA
Results: 1 to 1 of 7
 • Blitz the Ambassador

  Country  Ghana USA
  Genres urban hiphop fusion afrobeat
  Website blitz.mvmt.com
  FestivalSauti za Busara 2015
  Recordings

  Diasporadical EP (2015); Afropolitan Dreams (2014); The Warm Up EP (2013); Native Sun (2011); Stereotype (2009); Double Consciousness EP (2005); Soul Rebel EP (2004)

  Blitz the Ambassador - All Around The World / Respect Mine ft. Emicida & Y'akoto

  Blitz the Ambassador
  Blitz the Ambassador

  ‘Nilihitaji stori ambayo si yenye mvuto wa kudanganya, lakini iliyogusa changamoto za vijana wahamiaji kiukweli’, anasema Blitz the Ambassador kwenye albam yake ya hivi karibuni, Afropolitan Dreams. Ikiwa na maono ya kuukubali uafrika Magharibi wake na mabadiliko ya baadae, kijana mshehereshaji mwenye mipigo ya kiafrika, hadhi ya kimarekani, biti za kigumu na nyimbo alizoshirikiana na washirika wake wa kimataifa akiwemo Angelique Kidjo, Seun Kuti na Nneka. Lakini kama kawaida ya Blitz, albam zake huwa ni zaidi ya mziki, ni kuhusu wahamiaji ambao wameitengeneza Amerika. Kila mtu, kila kizazi, nakila mchukuzi wa tamaduni inayokuja kwa meli ama kwa ndege ikaleta hisia. Uhamiaji ni kiunganishi kinachounganisha mambo yaliyopita, ya sasa na yanayokuja.

   

  Afropolitan Dreams inaelezea muingiliano wa stori na matatizo ambayo Blitz the Ambassador anayajua kiundani zadi. ‘nilitoa stori kwenye albam yangu ya mwisho, Native Sun,’ akisema. ‘Hiyo ilikuwa safari yangu kuelekea America kutimiza ndoto zangu. Huu ulikuwa kama muendelezo, lakini wenye mambo mengi yaliyoanzia chini na kupanda juu. Afropolitan Dreams ilipendwa na mkusanyiko wa rika na nidhamu tofauti. Kitu tulichokuwa nacho muda huo ni kwamba wote ni wahamiaji.

   

  Blitz alifika Marekani mwaka 2001, akitokea Ghana, ambako alikulia akisikiliza mziki wa soul wa kimarekani, wenye hadhi ya juu nyumbani kwao, Afrobeat za Fela Kuti, na shule ya zamani ya hiphop Public Enemy, Rakim na KRS-One. Alikuwa yutayari kutimiza ndoto zake.

   

  Katika nyimbo za Blitz kila kitu hutolewa kutoka katika uzoefu mkali. Mara nyingi huwa na ubunifu mkubwa na uwasilishaji wa ujumbe, soundtrack ya Blitz iliifanya Afropolitan Dreams kuwakilisha dunia nzima.