4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Blick Bassy
Results: 1 to 1 of 1
  • Blick Bassy

    Country  Cameroon
    Genres band fusion jazz roots
    Website www.worldconnection.nl
    FestivalSauti za Busara 2011
    Recordings📼

    Léman (2008)

    Blick Bassy - Donalina

    Blick Bassy
    Blick Bassy

    Blick Bassy ni sauti ya kinafsi (soul) ya Cameroon - nafsi kwa maana ya  kwamba sauti anayoimba hutokea ndani ya roho. Katika albamu yake ya hivi karibuni mwimbaji, mtunzi, mpiga gitaa na mpiga tumba ameuchukua muziki wa Afrika ya kati  na Afrika Magharibi na kuuchanganya  na mtindo ya Bossa nova, jazz na soul. Gitaa la Bassy huchezwa na kwa mtindo wa kiana ambao huwalevya mashabiki, sauti laini za waimbaji na utajiri wa kora vilevile ala za kiasili kama vibuyu na bass husababisha sauti ya kipekee, ambayo  huleta miondoko ilio Groovy. Léman(2008) ni album yake ya kwanza iliorekodiwa katika studio  za Salif Keita huko Bamako, Mali. Bassy kiongozi wa sasa anaishi Paris, Ufaransa. "Léman maana yake ni kioo” anaelezea Blick. Anaendelea “kioo ni huakisi jamii. Na unaweza pia kuona nyuma yenu kwa kutumia kioo.”

     

    Bassy alizaliwa mwaka 1974, pamoja na ndugu zake 10 katika mji mkuu wa Cameroon, Yaoundé. Akiwa na umri wa miaka 10, Bassy alipelekwa kuishi na babu yake kwa miaka miwili huko Mintaba, kijiji kidogo katikati ya Cameroon. Babu yake alimlea Bassy kwa desturi na utamaduni, na mafunzo ya aina mbalimbali ya kazi, kama vile uvuvi, uwindaji na kilimo. Vilevile alimfundisha elimu ya muziki. Huko Mintaba, wanakijiji hawapendelie kufanya mazungumzo mengi lakini zaidi hupendelea sana kuimba wakati kazi zao za kila siku. Mama yangu alikua akimba kuanzia asubuhi mpaka usiku. Yeye ni mmoja wa watu walionipa moto wa matarajio kimuziki na ndiye alienifundisha jinsi ya kuimba. “Nilianza kwa sikiliza wanamuziki kama Marvin Gaye, Gilberto Gil na Nat King Cole.” Nilitambua mapema kuanilitaka kuchanganya uzuri wa utamaduni wangu wa Bassa na mila zake za muziki na hivyo kuniwezesha kuujenga muziki wangu soulful". Tangu 2005 Bassy alipohamia Paris, kashafanya kazi na Manu Dibango, Cheikh Tidiane Seck, Lokua Kanza na Etienne Mbappé.

    CULTURESFRANCE-100
    With thanks to CULTURES FRANCE