4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Mgodro Group
Results: 1 to 1 of 1
  • Mgodro Group

    Country  Zanzibar
    Genres traditional roots
    Website www.zanzibarmusic.org
    FestivalSauti za Busara: 2015
    Mgodro Group
    Mgodro Group

    Wazo la kuanzishwa kwa kundi hili lilitoka kwa Matona ambaye alifikiria kurejesha ngoma za asili alizokuwa anacheza utotoni mwake: muziki huu unapigwa na na watu wenye asili ya Comoro ambao wanaishi Mji Mkongwe, Zanzibar. Shukrani ziende kwa Alliance Francaise and Japanese Trust kwa kufanikisha safari ya Matona kwenda Comoro ikiwa ni moja ya sehemu ya mradi wa  “Song of the Moon” ikiwa na lengo la kufufua Taarab katika hivi visiwa. Wakati yupo Comoro, Matona alipata nafasi ya kufanya manyesho na wasanii wakubwa: Bwana Riziki (Comoro) na Athuan Subira (Mayotte) walimgusa sana kimuziki. Bwana Riziki alimfundisha Matona kupiga Gambusi. Safari iliendelea mpaka Matona alipoalikwa mwaka 2012 kufanya onyesho Mayote chini ya mradi ‘Violins of Zanzibar’ ambapo alipata nafasi ya kufanya maonyesho na mtunzi na muimbaji maarufu wa taarab Lima Wilde. Kisha baadae akapata safari ya mjini  Marseille nchini Ufaransa, Matona alikutana na Ahamada Smis na  Athuan Subira kwa mara ya pili wote wenyeji wa Comoro pamoja na Lego mpigaji maarufu wa Kodian kutoka Madagasca. Wasanii hawa waliendelea kupanua wigo wa uelewa wa Matona hasa katika nyanja za muziki wa visiwani na ala zake. Kwa sasa Matona anawafundisha wanafunzi wa DCMA na hivi karibuni wataanza kutunga nyimbo zao.
     Kikundi cha Mgodro kilianzishwa mwaka 2003, ikiwa ni moja ya matunda ya mafunzo na mradi huo. Mgodro una mchanganyiko wa radha na mahadhi ya visiwani kama Comoro, Madagasca, Reunion, Mayote na Mauritious na yenye ngoma kama chakacha, mgodro, Salegy, Sega, maloya, chigoma, chumbadori na mbiwi. Watu mbalimbali walikuwa wanafurahia ngoma hizi hapa Zanzibar lakini hivi karibuni zimeanza kupotea na kusahauliwa. Kikundi cha Mgodro kilifanya onyesho lake katika tamasha la kimataifa la filamu (ZIFF) mwaka 2013, na sasa linafanya maonyesho kila wiki baadhi ya maeneo ya Zanzibar na Dar es Salaam. Kikundi kimeshanza kuwa maarufu na kupendwa na wengi.