4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Mkota Spirit Dancers
Results: 1 to 1 of 1
  • Mkota Spirit Dancers

    Country  Zanzibar
    Genres ngoma roots
    FestivalSauti za Busara 2012

    Mkota on Steroids

    Mkota Spirit Dancers
    Mkota Spirit Dancers

    Mkota Spirit Dancers ni kikundi cha ngoma za muziki wa asili kutoka Zanzibar katika kisiwa cha Pemba, hufahamika sana kama wasanii wenye juhudi na maarifa kutoka Zanzibar. Tangu mwaka 1985 wanaendelea kuwateka mashabiki kwa aina yao ya kipekee ya uchezaji ikiwemo gonga, kyaso, boso na aina yao ya uchezaji ijulikanayo kama kumbwaya. Upigaji wa ngoma na uchezaji wakiwa wamevaa mapembe ya ng’ombe.

    Maonyesho yao huwasafirisha kihisia watazamaji mpaka katika kisiwa cha Pemba chenye utajiri wa utamaduni. Kikundi chenye watu 13 watafanya onyesho katika tamasha la Sauti za Busara 2012, na wameahidi onyesho lao si la kukosa.

    Muonekano wao katika tamasha la Sauti za Busara umewezeshwa na Swahili Performing Arts Center ikishirikiana na ZanAir.