4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > Skuli ya Kiongoni
Results: 1 to 1 of 1
  • Skuli ya Kiongoni

    Country  Zanzibar
    Genres roots traditional
    FestivalSauti za Busara 2012
    Skuli ya Kiongoni
    Skuli ya Kiongoni

    Kikundi kinamilikiwa na shule ya msingi Kiongoni iliyopo kusini mwa Zanzibar kunakojulikana kwa jina la Makunduchi, kundi lilianzishwa rasmi mwaka 2001.

    Shule ina darasa maalumu kwa ajili ya mafunzo ya ngoma za asili, hufundisha aina ya ngoma tofauti kutoka zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

    Katika kufanikisha kuweka sifa yake nchi nzima kila mwaka shule ya kiongoni inaalikwa kufanya onyesho katika sherehe mablimbali. Mwaka 2006 walishiriki katika mashindano ya shule za zanzibar na kufanikiwa kushinda, mwaka uliofuata walialikwa na chama tawala kwa ajili ya kwenda kuwaburudisha wabunge katika bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania na mwaka 2009 walikwenda kuwaburudisha Meya katika mkoa wa Dodoma. Vilievile ni miongoni mwa vikundi vilivyoshiriki katika shindano la ngoma lililoandaliwa na Busara Promotions na kupata kupata nafasi ya kushiriki kwenye Tamasha.