4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: search > TaraJazz
Results: 1 to 1 of 1
 • TaraJazz

  Country  Zanzibar
  Genres jazz
  Website zanzibarmusic.org
  Facebook /TaraJazzZanzibar
  FestivalSauti za Busara 2019, 2020, 2021
  Recordings

  Machozi, 2017

  Kama 'ulimiss' taarabu asilia waweza sikiliza hii

  TaraJazz
  TaraJazz

  Bendi hii ya vijana wenye kusisimua inajumuisha wachunguzi katika masuala ya kimuziki, kufuatilia, kujiongeza na kwenda na aina mpya ya muziki. Msingi wao ni muziki wa jazz wenye mchanganyiko na Taarab. TaraJazz wameweza kuteka nyoyo za watu kwa ubunifu wao wa kipeke na wa kusisimua, muunganiko wa vionjo vya taarab ya Zanzibar vikienda sambamba na jazz pamoja na ladha mbalimbali za muziki wa Kitanzania na kiafrika kwa ujumla.

   

  "Hii ni sauti mpya duniani" alisema Hassan Mahenge (mchezaji wa oud, saxofoni na ngoma). "Ni afrojazz, ni tarajazz, ni harakati ya muziki ambao daima unakua kwenda sehemu nyingine. “Japokua hatujui safari hii itatuchukua mpaka wapi ila tunaamini lazima sehemu hiyo itakua nzuri na mahususi kwetu”