Sarabi
Country Kenya Genres band urban rock reggae Website /pages/SARABI/260804687286737 Festival Sauti za Busara 2015, 2017 Recordings 📼 Oyaore (album), 2013 ; Suluhisho (single), 2013; Toto Africa (single), 2013 ; Fuata Sheria (single), 2013
Gazeti la Buzz liliisifu Sarabi kama“nyuso mpya za muziki wa kisasa wa kiafrika kutoka Kenya”.
Sarabi iliundwa mwaka 2005, kwa miaka ya karibuni, Sarabi wamekuwa ni wasanii wanaoheshimika kutoka Kenya. Kikundi hichi kina wasanii wanane wanaotoka sehemu za kimasikinisana huko Kenya. Walianza kupiga muziki pamoja wakiwa wadogo kama na umri wa miaka kumi na moja tu.
Muziki wao unatokana muziki wabenga, ukichanganyika na muziki wa Ulaya. Mwaka 2013, alitoa albamu yaoinayoitwa Oyaore. Mwaka 2014, walitoa albamu yao ya Sheria ambayo ilimjumuisha muimbaji Juliani pia, wimbo huu ulipendwa sana kwa vile ulikuwa unazungumzia kuhusu sakata la mahindi, pia kuhusu kulipia ada za shule, ukosefu wa kazi kwa vijana na jinsi rushwa ilivyotawala kwenye jamii.
Sarabi ni wanamuziki wachangamfu sana wanapokuwa jukwaani. Wamewahi kuja kwenye tamasha la Sauti za Busara mwaka 2015, pia walikwenda Ethiopia kwenye tamasha la Selam, na tamasha la Bayimba huko Kampala. Walishiriki DOADOA na pia kwenye maonyesho mbalimbali huko Dar es Salaam.
Mwaka 2015 walifanya maonyesho kadhaa huko bara la Ulaya, walishiriki tamasha la Africa Oye linalofanyika Liverpool nchini Uingereza. Na walishiriki kwenye tamasha la WOMEX mwaka huo huo.
with thanks to Africalia
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava