Babawatoto Centre
Country Tanzania Genres acrobats Website babawatotofitforlife.net Festival Sauti za Busara 2015 Kituo cha watoto cha Babawatoto Centre kilianzishwa mwaka 2006 Makurumla, katika kitongoji kinachoishi watu wengi jijini Dar es Salaam. Mwanzilishi ni Mr. Mgunga Mwa Mnyenyelwa, mtendaji maarufu wa sanaa za maonesho ambaye pia alianzisha shirika maarufu ya maonesho Parapanda Theatre. Babawatoto Centre ina lengo la kuwawezesha vijana na jamii zilizokandamizwa ili waweze kushinda changamoto mbalimbali kama za upendeleo wa kijinsia, umasikini, uhalifu na magonjwa. Babawatoto ina muono wa jamii yenye watoto huru na walio mbali na unyanyasaji Tanzania.
Babawatoto ni shirika bunifu linatotumia njia shirikishi ikiwemo sanaa za maonesho na sarakasi. Zaidi ya watoto 80 wanashiriki katika sarakasi, sanaa ya trapezi, juggling na ngoma za samba reggae vimewaongezea uwezo ndani ya Babawatoto.
Babawatoto hutumia sarakasi kama nyezo ya kutoa ufahamu kwa jamii kuhusiana na watoto wa mitaani. Maonesho ya kuigiza ya mtaani huvutia watoto kwenda Babawatoto Centre badala ya kucheza majalalani. Maonesho yao njia ya kipekee ya kuburudisha ambayo huburudisha watu wa rika zote na tamaduni tofauti.
with support from CEFA Tanzania
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava