Mgodro Group
Country Zanzibar Genres traditional roots Website www.zanzibarmusic.org Festival Sauti za Busara: 2015 Wazo la kuanzishwa kwa kundi hili lilitoka kwa Matona ambaye alifikiria kurejesha ngoma za asili alizokuwa anacheza utotoni mwake: muziki huu unapigwa na na watu wenye asili ya Comoro ambao wanaishi Mji Mkongwe, Zanzibar. Shukrani ziende kwa Alliance Francaise and Japanese Trust kwa kufanikisha safari ya Matona kwenda Comoro ikiwa ni moja ya sehemu ya mradi wa “Song of the Moon” ikiwa na lengo la kufufua Taarab katika hivi visiwa. Wakati yupo Comoro, Matona alipata nafasi ya kufanya manyesho na wasanii wakubwa: Bwana Riziki (Comoro) na Athuan Subira (Mayotte) walimgusa sana kimuziki. Bwana Riziki alimfundisha Matona kupiga Gambusi. Safari iliendelea mpaka Matona alipoalikwa mwaka 2012 kufanya onyesho Mayote chini ya mradi ‘Violins of Zanzibar’ ambapo alipata nafasi ya kufanya maonyesho na mtunzi na muimbaji maarufu wa taarab Lima Wilde. Kisha baadae akapata safari ya mjini Marseille nchini Ufaransa, Matona alikutana na Ahamada Smis na Athuan Subira kwa mara ya pili wote wenyeji wa Comoro pamoja na Lego mpigaji maarufu wa Kodian kutoka Madagasca. Wasanii hawa waliendelea kupanua wigo wa uelewa wa Matona hasa katika nyanja za muziki wa visiwani na ala zake. Kwa sasa Matona anawafundisha wanafunzi wa DCMA na hivi karibuni wataanza kutunga nyimbo zao.
Kikundi cha Mgodro kilianzishwa mwaka 2003, ikiwa ni moja ya matunda ya mafunzo na mradi huo. Mgodro una mchanganyiko wa radha na mahadhi ya visiwani kama Comoro, Madagasca, Reunion, Mayote na Mauritious na yenye ngoma kama chakacha, mgodro, Salegy, Sega, maloya, chigoma, chumbadori na mbiwi. Watu mbalimbali walikuwa wanafurahia ngoma hizi hapa Zanzibar lakini hivi karibuni zimeanza kupotea na kusahauliwa. Kikundi cha Mgodro kilifanya onyesho lake katika tamasha la kimataifa la filamu (ZIFF) mwaka 2013, na sasa linafanya maonyesho kila wiki baadhi ya maeneo ya Zanzibar na Dar es Salaam. Kikundi kimeshanza kuwa maarufu na kupendwa na wengi.
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava