Kiki Kidumbaki
Country Zanzibar Genres kidumbak taarab traditional Website www.zanzibarmusic.org Festival Sauti za Busara: 2015 Katika miaka ya 1950 sehemu nyingi za Zanzibar ikiwemo mitaa ya Mji Mkongwe kulikuwa na angalau kikundi cha Taarab au Kidumbaki. Kwa bahati mbaya vimebaki vichache mno. Hata hivyo katika kijiji cha Mahonda nje ya Mji Mkongwe, njia ya kuelekea Kaskazini mwa Kisiwa cha Unguja, ndipo panapopatikana kikundi cha KIKI KIDUMBAKI kilichoanzishwa tangu mwaka 1993.
Miaka kumi iliyopita kiongozi wa Kikundi, marehemu Ali Baramia alimfuata Hilda Kiel ambaye alikuwa kiongozi wa Chuo cha Mziki Zanzibar (DCMA) alimuomba msaada wa kuendeleza sanaa ya mziki kwenye kikundi. Matokeo yake palifunguliwa tawi la Chuo cha Mziki (DCMA) chini ya udhamini wa UNESCO kwa kusaidia kufundisha walimu na wasanii na kununua vifaa na kufanyia matengenezo ya jengo la chuo na mahitaji mengine. Katika hali hiyo KIKI TAARAB kiliweza kufanya maonyesho yake mara nyingi ndani ya DCMA, Mji Mkongwe na Mahonda lakini tangu udhamini ufikie kikomo DCMA ilikuwa inahangaika kutafuta pesa kwa ajili ya kukiendeleza kikundi.
Kwa bahati nzuri wasanii waliweza kukiendeleza kikundi. Mkurugenzi wa Sanaa wa DCMA, Matona Mohammed anajitahidi kuboresha uwezo wa kufanya maonyesho kwa vikundi vyote vya DCMA. Katika hali hiyo kikundi kinafanya maonyesho ya kila wiki sehemu mbalimbali kama Old Dispensary, Gymkhana Club, na baadhi ya maeneo ndani ya Mji Mkongwe. KIKI kimefanikiwa kujizolea sifa ya kuwa kikundi bora cha Kidumbaki tofauti na vikundi vingine vinavyopunguza radha asilia za kidumbaki.
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava