Afrijam Band
Country Tanzania Genres fusion jazz reggae Website /Misoji-Nkwabi-and-Afrijam-1520448294936766 Festival Sauti za Busara 2017 Recordings 📼 Utu wa Mtu 2009; Usawa 2014
Misoji Nkwabi alijinyakulia ushindi wa Bongo Star Search hapo mwaka 2008 na kurekodi albamu yake inayoitwa Utu wa Mtu. Albamu hii ilikuwa na nyimbo kumi na mbili zikiwa zote zinagusia maisha ya kisasa yanayowakumba vijana wa kitanzania, hususan kwenye mambo ya kijamii na kiafya kama vile maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Misoji alianza kuimba akiwa mdogo sana kwenye kundi la kwaya la kanisani, ambapo mama yake alikuwa ni mpigaji wa ala ya muziki. Baadae alianza kuimba nyimbo za wasanii tofauti na hatimae akawa ni mtunzi wa mashairi yake mwenyewe.
Mwaka 2014 aliunda Kikundi cha mziki cha Afrijam, ambacho kilishiriki kwenye matamasha tofauti nchini Tanzania kama vile Karibu Music Festival, Marahaba Festival na Tamasha la Bagamoyo.
Mwaka 2009, Misoji alishirikiana naMombots Production kwenye filamu ya muziki huko nchini Ujerumani. Yeye ana shahada ya sanaa ya maigizo ambayo alisomea chuo cha sanaa TASUBA huko Bagamoyo.
Kwenye kikundi hichi, Misoji anaimba na wadogo zake wawili, Nsami na Nshoma.
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava