H_art the Band
Country Kenya Genres band Website www.penya-africa.com Festival Sauti za Busara 2017 Recordings 📼 2004 Nikikutazama; 2015 Lovephobic
H-Art the Band ni kikundi cha wasanii watatu Mordecai Kimeu, Kenneth Muya na Wachira Gatama. Walikutana walipokuwa wakifanya mazoezi ya kuingia kwenye sanaa ya uigizaji mwaka 2012 huko kwenye jumba la Taifa la Sanaa ya Maigizo, Kenya. Wakati wakifanya mazoezi walijikuta wote wanapenda muziki, mashairi, sanaa ya vichekecho, ngoma na hadi mtazamo wao wa kimaisha unafanana. Hivyo wakakubaliana kuunda kikundi chao cha H-art the band, baada ya hapo wakajiunga na program ya Sauti Academy ambapo walihitimu mwaka 2014.
Sanaa ya H-art the band ni mchanganyiko wa nyimbo nyororo, mashairi, rap, uigizaji, ngoma na pia mitindo ya mavazi. Sanaa na muziki wa kikundi hichi inapendwa na watu wa rika zote. Mordeci na Wachira wao ni washairi na waimbaji na Kenchez ni mpigaji kinanda cha guitar.
Kwa kipindi cha mwaka uliopita, H-art the band walikuwa wakifanya maonyesho mfululizo, kila sehemu na hadi majiani. Hivyo, hili limewajengea ukakamavu na umashuhuri kwenye jukwaa la muziki nchini Kenya.
with thanks to Africalia
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava