Lumumba Theatre
Country Tanzania Genres acoustic band dance fusion Festival Sauti za Busara 2012, 2013 Lumumba Theatre ni kikundi chenye vijana wenye vipaji katika fani uimbaji, uigizaji na muziki. Lumumba ilianzishwa mwaka 1997 na kiongozi wa kundi hilo Djuto Komba alianza na kuwakusanya vijana wenye vipaji kutoka katika Shule ya Msingi ya Lumumba iliyopo maeneo ya Mnazi mmoja ndani ya jiji la Dar es Salaam. Lumumba wanauchu wa mabadiliko na maendeleo ya kijamii. Katika kulishughulikia hilo wanahamasisha vijana kwa kutoa mafunzo ya uchezaji ngoma, maonyesho na muziki, na kutoa nafasi kwa vijana kusoma, kuonyesha ubunifu wao na kuufanyia kazi. Lumumba wameshafanya maonyesho nchi mbalimbali kama Kenya, Uganda, Msumbiji, Ujerumani, Denmak, India na Poland.
Kipindi cha mwanzo waliangazia ngoma za asili za Tanzania, kwa sasa wamefanya mseto wa shughuli tofauti na kutoa semina ya uchezaji, kuandaa maonyesho, uandishi wa hadithi na muziki wa Afrika.
Wanatumia vifaa tofauti kama Sexaphone, Filimbi, Marimba, Kinanda na Gitaa, na ni kikundi chenye nidhamu, uzoefu katika ngoma za asili na za kisasa. Huwa hawachoshi kuwaangalia wawapo jukwaani na kuhakikisha kila mtu anaridhika na wanachokifanya.
Walifanya onyesho la nguvu katika tamasha la busara 2012 na umati wa watu uliwashangalia na kusema wameleta changamoto kwa vikundi vya Tanzania.
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava