4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
> Sibusiso
Results: 2 to 2 of 408
 • Abantu Mandingo

  Country  Tanzania
  Genres fusion
  FestivalSauti za Busara 2014

  Abantu Mandingo
  Abantu Mandingo

  Swahili Ally ni kijana wa kitanzania mwenye kipaji cha utunzi na uimbaji wa muziki, mzaliwa wa mkoa wa Tanga mwaka 1989, na alipata elimu yake msingi katika shule ya Kigambini alipoanzia shunguli za muziki. Babu yake alikuwa mwanamuziki na ndiye aliyekuwa anamfundisha muziki, baada ya babu yake kufariki bibi yake ndiye anayemshauri masuala ya muziki kwa sasa.

   

  Anatokea katika kabila maarufu katika mkoa wa Tanga "Wadigo" ambapo huimba kwa lugha ya kidigo anachangnya na Kiswahili. Ni mmoja kati ya vijana anayejitahidi kufanya ubunifu katika sanaa na kufanya maonyesho yake yawe yenye kukumbukwa pindi kila anapofanya onyesho. Mwaka 2005 ndipo alipojiingiza rasmi kwenye muziki na mwaka 2009 akaanza kusikika katika tasnia ya muziki.

   

  Mwaka 2010 alijiunga na kundi la Ngoma za Asili "Lumumba Theatre" lenye makazi yake jijini Dar es Salaam, kundi hilo liliweza kumpatia uwezo wa kujiamini zaidi katika mambo ya muziki ambapo aliweza kusafiri sehemu mbalimbali kama Music Crossroad na Umoja Cultural flying carpet nchini Msumbiji na Sauti Academy nchini Kenya.

   

  Vilevile mwaka 2012 alipata fursa ya kufanya maonyesho na wasanii kutoka sehemu mbalimbali kama Afrika ya kusini, Uganda, Kenya, Norway, Zimbabwe na Ethiopia katika tamasha la Umoja lililofanyika nchini Msumbiji. Usikose kumuona akipanda jukwaani akiwa na Abantu Mandingo katika tamasha la Sauti za Busara mwaka 2014.