Results: 12 to 12 of 15
Comrade Fatso & Chabvondoka
Country Zimbabwe Genres band fusion hiphop reggae Website www.comradefatso.com Festival Sauti za Busara 2009, 2013 Recordings 📼 House of Hunger, 2008; Korokoza (single), 2011
Comrade ni mkali wa mashairi kutoka Zimbabwe. Amejifunza mambo mengi ya muziki katika nchi tofauti kama Marekani, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa. Maranyingi hujitahidi kuwaburudisha na kuwatolea ujumbe mashabiki wake.
Comrade na bendi yake ni kikosi kazi chenye kutoa radha tofauti za muziki kama Rock, hip hop, chimulenga, jit, kwaito na reggae. Walitoa albamu waliyoipa jina la nyumba ya njaa (House of hunger) lakini bahati mbaya ilipigwa marufuku nchini Zimbabwe kutokana na hali ya kisiasa. Wameshafanya maonyesho ndani ya bara la ulaya, Marekani, Karibiani na Afrika. Mwaka 2010 walifanya onyesho katika tamasha kubwa lijulikanalo Exit Festival.
Comrade alifanya ziara tena katika bara la ulaya mwaka 2011 katika tamasha la Uppsala International Poetry Festival nchini Sweden na ziara ndefu ya mwezi mzima nchini Denmark. Albamu ya hivi karibuni ijulikanayo kama Korokoza imefanikiwa kupata sifa ulimwengu mzima kutokana na maudhui yake na mpangilio wa mashairi ambayo ni adimu katika masikio ya watu wengi.