4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Genre > rock
Results: 15 to 15 of 15
 • The Brother Moves On

  Country  South Africa
  Genres roots rock urban fusion
  FestivalSauti za Busara 2015
  Recordings

  The Golden Wake (2010); E.T.A Expected Time of Arrival (2012); A New Myth (2013)

  The Brother Moves On [@ the assembly '13]

  The Brother Moves On
  The Brother Moves On

  The Brother Moves On ni mkusanyiko wa muziki wa majaribio kutoka Johannesburg, Afrika Kusini, wakichanganya muziki wa rock, Xhosa funk, jazz, folk, electronic, dansi na maneno katika kipindi baada ya ubaguzi wa rangi. Bila kuweza kuwekwa katika mgawanyo wowote, wanapendelea kujitambua kama aina ya muziki wa baadae.


  Kundi liliundwa mwaka 2010 na msanii wa maeneo tofauti Nkululeko Mthembu. Walianzisha harakati waliyoipa jina binafsi ambao ulikua kwa kiasi kikubwa na wasanii wakigrafiki na sanaa za mikono na baadaye waliijumuisha wapiga vifaa wa muziki kwa ajili ya mazingira ya mziki wa moja kwa moja (live).


  Jina la The Brother Moves On ni mkanganyiko wa kisarufi wa The Brother Mouzone, ya mhusika wa kuundwa katika televisheni ya tamthiliya ya Kimarekani The Wire. Katika hatua zao za kuchipukia, harakati hiyo iliuliza kuhusu dhana hiyo ambapo kila mwanachama alikua katika hatua na wahusika wa muda mfupi katika  mchakato. Hivyo ndipo lilipotoka  jina hilo The Brother Moves On.


  The Brother Moves On [inayofupishwa kama TBMO] ni kundi linatumbuiza sanaa ya moja kwa moja (live).  Muziki wao sio mweupe au mweusi, lakini ni wazi kwamba una chimbuko lake Afrika Kusini,  ukinyonya kutoka katika utajiri wa nchi yake katika historia ya kisiasa – kitu ambacho kinakua wazi wakati unasikiliza ufafanuzi wao wa kijamii. Wanaunda katika maneno yao, “muziki wa mpito kwa ajili ya kizazi cha mpito”, kwa maneno mengine, muziki kwa ajili na kuhusu ambapo kizazi cha Afrika Kusini kilichozaliwa baada ya ubaguzi wa rangi ambacho ni huru na chenye matumaini, lakini pia kilichoangushwa na kuathiriwa na mfumo ambao haujafikisha mengi kusaidia matarajio ya kizazi  hiki, haswa matarajio ya wale wasio na kitu.


  Bendi hii ipo katika muono wa muziki halisi wa Johannesburg na ilikua bendi ya kwanza kufanya tamasha la Firefest Route na kufanikiwa kufanya maonyesho kwenye matamasha mbalimbali kama Msumbiji, Swaziland, Botswana na visiwa vya Reunion. Umaarufu wa kimataifa unakua, pamoja na TBMO kuwakilisha Afrika Kusini,  Ufaransa, Uingereza, Ujerumani na katika tamasha la Oslo World Music Festival nchini Norway. Cha kuvutia zaidi bendi imefanya hivi wao wenyewe:  wakajisimamia wenyewe, wakirekodi wenyewe.  Mwaka 2014 The Brother Moves On ilikua moja ya bendi changa kuwa na nyimbo iliyopigiwa kura kuwa  katika Nyimbo Bora 100 Afrika Kusini.
   

  SDC_LOGO_2007
  With thanks to SDC