4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: A - Z > U
Results: 3 to 3 of 5
  • Usambara Sanaa Group

    Country  Tanzania
    Genres traditional
    FestivalSauti za Busara 2017
    Usambara Sanaa Group
    Usambara Sanaa Group

    Kikundi hichi ni cha wasambaa na muziki wao ni wa asili ya wasambaa kutoka Lushoto na Korogwe huko Tanga. Wasanii wote wa kikundi hiki ni wakaazi wa Dar es Salaam.

    Dhumuni kubwa la kikundi hiki ni kudumisha mila na sanaa za muziki na ngoma ya wasambaa ijulikanayo kama Mdumange. 

    Mdumange ni ngoma inayopigwa wakati wa furaha kama vile wakati wa harusi, wakati wa mavuno na pale wageni wanapokuja kuwatembelea wasambaa.  Ngoma hii inachezwa kwa mduara na huwajumuisha watu wote kusherehekea.

    Ala zinazotumika kupiga Mdumange  ni ngoma moja ndogo amboayo ndio inayoanza kupigwa pia kuna ngoma kubwa sita, na ngoma moja ya bati la aluminium hizi zote hupigwa na mtu mmoja.  Wasanii waliobakia huimba na kucheza.