4 A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
Artists: Festival Line-up > 2022
Results: 5 to 5 of 19
 • Siti & the Band

  Country  Zanzibar
  Genres taarab kidumbak roots pop fusion
  Website sitiandtheband.com
  Facebook /sitiandtheband
  FestivalSauti za Busara 2018, 2020, 2022
  RecordingsFusing the Roots, 2018
  On stage Feb 2022

   Sat 12,  11:50pm Old Fort Main Stage

  Siti & the Band ft. G Nako - Uchungu wa Mwana (Official Music Video)

  Siti & the Band
  Siti & the Band

  Siti & The Band ni wana mabadiliko ya muziki ambao wanachanganya muziki wa asili wa Zanzibar na wa kisasa ikiwemo Jazz, funk na rege pamoja vionjo vingine.

  Amina Omar aka Siti Amina na bendi yake wamevutia sana na Siti bint Saad and Bi Kidude, hawa ni akina mama wa Taarab ya Zanzibar. Katika kuuenzi na kuuendeleza urithi wao, bendi hii imekuwa mfano wa kuigwa katika kizazi kipya cha muziki wa Afrika Mashariki, kufurahia asili yao, kuthamini upekee na kutengeneza utambulisho katika kutafuta muziki wao. Suala la msingi zaidi, Siti anapigania haki za wasani wenzake wa kike katika kujieleza ili wasikike kwenye masuala ya unyanyasaji.

  Albamu ya mwanzo ya Siti & The Band ‘Fusing the Roots’ imeonyesha kutokuwa na wakati wa muziki wa asili na wa kisasa. Mashairi yenye nguvu yaliyotoa mwanga wa kujitegemea wa Mwanamke wa Afrika. Mpangilio wa muziki ulioendana sanjari na na radha za asili na za kisasa. Tungo zilizochanganywa na jumbe za uwezeshaji, albamu hii imetafsiri urithi wa utamaduni kwa jamii ya sasa.