Results: 6 to 6 of 6
Trio Kazanchis +2
Country Ethiopia Switzerland Genres jazz traditional other Website www.121234.net Facebook /Kazanchismusic Festival Sauti za Busara 2019 Recordings 📼 Amaratch Musica, 2012; Dinkenesh, 2014; Sheger, 2018
Mwaka 2008, Jeroen Visser (Switzerland) alijikuta akiwa na Mesele Asmamaw (Ethiopia) na Fabien Duscombs (Ufaransa) katika kumbi mbalimbali mjini Addis Ababa. Umeme uliwaka na wakajikuta wanaanzisha kundi lao walilolipa jina la Trio Kazanchis, palepale katika wilaya inayokutanisha vipaji vya muziki na wachezaji.
Trio Kazanchis walitoa albamu yao ya kwanza Amaratch Musica mwaka 2012 kupitia lebo ya Ethio-Sonic ya Buda Musique, studio inayojulikana kwa kutoa mfululizo wa nyimbo za Ethiopia.
Waliutambulisha kwa kuuandika muziki wao kama 'Ethiopian traditional impro punk’ wakati wadau wa muziki wa Kiafrika waliutaja kama Jazz ya Kiafrika. Walifanya ziara ya kimuziki nchini Uswisi, Ufaransa, Uholanzi, Ubelgiji, Jamhuri ya Czech na China. Katikati walirudi Ethiopia kwa ziara ya kimuziki sehemu ambayo walikutana na kuanzisha kundi lao na kupiga Kazanchis tena. Endris Hassen, mmoja wa wachezaji bora wa Ethiopia aliyejiunga na kikundi hicho, hivyo Trio Kazanchis ilipanuliwa kama Trio Kazanchis +1. Hii imesababisha albamu yao ya pili 'Dinkenesh' iliyotolewa mwaka wa 2014. Albamu yao ya tatu, yenye jina la 'Sheger', inaandaliwa kwa sasa inategemewa kutolewa hivi karibu.
With thanks to Pro Helvetia & SDC