Press Kiswahili Message

 
From: "Press Kiswahili" <pressnewsletter_sw@PROTECTED>
Subject: Press Kiswahili Message
Date: February 9th 2022

 

 

 

 

Taarifa kwa vyombo vya habari

Februari 11, 2022

Sauti za Busara 2022 inaanza leo

 

Zanzibar. Sauti za Busara, moja ya tamasha zinazoongoza barani Afrika, inaanza leo Ngome Kongwe, Stone Town huku wasanii mbalimbali kutoka Tanzania na sehemu nyingine za Afrika wakitarajia kutumbuiza mubashara.

Mbali na vikundi vinne vilivyo wahi kutumbuiza katika tamasha hilo, vingine vyote vinashiriki tamasha hilo kwa mara ya kwanza.

Akizungumza mjini Zanzibar siku ya Alhamisi, Mkurugenzi wa tamasha hilo Yusuf Mahmoud amewataka Watanzania na wageni waliotoka kila pembe ya dunia kujumuika kwa wingi kushuhudia na kushiriki tamasha hilo la kipekee.

Leo, tunaanza tukio la kipekee na la ajabu wakati Zanzibar inakaribisha siku tatu za 100% ya muziki mubashara wa Kiafrika. Tunajivunia hasa programu ya tamasha la mwaka huu, ambalo kwa hakika ni la kiwango cha kimataifa na mitindo mbalimbali ya muziki ili kuridhisha watazamaji wa rika na asili zote,” alisema Yusuf Mahmoud.

Aliongeza: "Miaka miwili iliyopita ilikuwa miaka ya kusikitisha kwa wasanii, tasnia ya ubunifu na utalii wa kitamaduni kwa sababu ya janga la Uviko-19. Sauti za Busara inawezekana ndilo tamasha pekee la muziki la Kiafrika ambalo liliendelea kufanya kazi, likionyesha uthabiti na wepesi katika kuunga mkono wasanii, huku likitilia mkazo uwezo wa muziki kuweka matumaini hai.”

Kwa kutambua changamoto wanazokabiliana nazo wasanii wa kike kote Tanzania na kwingineko, tamasha la mwaka huu lina kauli mbiu inayosema ‘Paza Sauti’.

"Tamasha letu linazingatia sana uteuzi wa wasanii wa kike, kuhimiza uwepo wao jukwaani na nyuma ya pazia. Pia tunatoa kipaumbele kwa wasanii wanaotumia muziki wao kuendeleza amani, umoja, haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na kuheshimu tofauti za kitamaduni,” aliendelea.

Safu ya wasanii watakaotumbuiza mwaka huu ni pamoja na Sampa The Great (Zambia), Siti & The Band (Zanzibar), Msaki na Nomfusi (Afrika Kusini), Suzan Kerunen (Uganda), Fanie Fayar (Congo- Brazzaville), Upendo Manase na Bahati Female Band (Tanzania). Wengine ni pamoja na Sjava (Afrika Kusini), Zan Ubuntu na Nadi Ikhwan Safaa (Zanzibar), Ben Pol, Sholo Mwamba, Vitali Maembe na Wamwiduka Band (Tanzania), Sylent Nqo na Evans Pfumela Mapfumo (Zimbabwe) na wengineo.

 

Tamasha la 19 la Sauti Za Busara linaloanza Februari 11 mpaka 13, 2022 linawezeshwa na Ubalozi wa Norway, Umoja wa Ulaya, CRDB, Zarlink, Emerson Zanzibar na wengineo.

 

Masharti na taratibu za usalama za Uviko 19 zitaendelea kuzingatiwa. Wataalam wa afya watakuwapo eneo la tukio pale inapohitajika. Waandaaji wanaendelea kufanya mapitio na kushirikiana na mamlaka za ndani na kuahidi kusimamia afya na usalama kwa wale wote wanaoshiriki au kuhusika na tamasha.

 

Kwa picha nk. tembelea: https://www.flickr.com/photos/sautizabusara2022/ & https://www.busaramusic.org/downloads/

 

  • This mailing list is a public mailing list - anyone may join or leave, at any time.
  • This mailing list is announce-only.

Orodha hii ya kutuma barua imekusudiwa tu kueneza habari zinazohusu Tamasha la Sauti za Busara kwa vituo au vyombo vya habari

Privacy Policy:

Sera faragha ya, Busara Promotions Press : Barua pepe zote katika orodha hii itatumika kwa madhumuni ya kukujuza shughuli zote zinazoendelea Busara Promotions. Hazitatolewa wala kupewa mtu mwingine au taasisi yeyote.