Press Kiswahili Message

 
From: "Press Kiswahili" <pressnewsletter_sw@PROTECTED>
Subject: Press Kiswahili Message
Date: February 10th 2023

Sauti za Busara kuanza leo na vipaji vya nyumbani

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Februari 10, 2023

Unguja. Baada ya miaka 19 ya mafanikio, Sauti za Busara, moja ya matamasha bora barani Afrika, leo Ijumaa Februari 10 katika eneo la Ngome Kongwe, Stone Town, Sauti za Busara itashuhudia toleo la 20 tangu kuanzishwa kwake.

 Kikundi cha DCMA Young Stars, ambao ni watoto wadogo wenye vipaji kutoka shule tofauti visiwani Zanzibar litalinatarajia kutumbuiza na wanamuziki na walimu kutoka Chuo cha Muziki cha Dhow Countries cha Zanzibar.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud, leo ni siku ya kwanza kati ya siku tatu za kusherehekea muziki wa Kiafrika na utofauti wa kiutamaduni huku wasanii mbalimbali kutoka barani Afrika wakipamba katika majukwaa mawili.

Mbali na majukwaa mawili ndani ya Ngome Kongwe, kwa mara ya kwanza, tamasha hilo pia Jumamosi Februari 11, litaandaa maonyesho kadhaa ya bila malipo wakati wa mchana katika Mji wa Fumba, mradi ulio chini ya CPS.

Akizungumza visiwani Zanzibar, Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud amewataka Watanzania kujumuika na wageni wengi ambao tayari wamefika kutoka kila pembe ya dunia kushuhudia na kushiriki katika tamasha hilo la kipekee.

"Leo, tunaanza kwa uzoefu wa kipekee na wa ajabu wakati Zanzibar ikiandaa siku tatu zitakazobeba asilimia 100 ya muziki wa Kiafrika. Tunajivunia kwa mwaka huu kuadhimisha tamasha la 20, tukiwa na orodha bora zaidi ya wanamuziki itakayowaridhisha wahudhuriaji kutoka katika kila kona ya dunia,” anaeleza Yusuf Mahmoud.

Kwa mujibu wa Bw. Mahmoud, miongo miwili ya burudani imefanya Sauti za Busara kuwa moja ya matamasha yanayoheshimika zaidi ya muziki wa Kiafrika ambayo imeendelea kufanyika, hata katika miaka yote ya changamoto ya janga la Uviko-19.

“Kwa miongo miwili sasa, tumeonyesha uthabiti na wepesi katika kusaidia wasanii, huku tukisisitiza nguvu na ushawishi wa muziki itumike kukemea ya maovu katika jamii yetu.

Kwa kutambua ukweli kwamba Afrika ni bara kubwa lenye historia na tamaduni tofauti na matarajio ya pamoja, onyesho la mwaka huu linafanyika chini ya kaulimbiu ‘Utofauti Wetu ni Utajiri Wetu.’”

Akizungumzia baadhi ya wasanii waliyowahi kupamba jukwaa la Sauti za Busara, meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhan aliwataja baadhi ya wasanii ambao maonyesho yao yaliacha gumzo kwa miongo miwili iliyopita.

“Tumeandaa matamasha na kuwa na mamia ya vikundi, lakini kuna wale amabo wmeacha gumzo kwa mfano, mwanamuziki mkongwe kutoka Zanzibar Marehemu Bi Kidude, Sampa The Great (Zambia), Nneka (Nigeria), Bassekou Kouyate (Mali), Blitz the Ambassador (Ghana), Sarabi (Kenya), Samba Mapangala (DRC), Ba Cissoko (Guinea), Sholo Mwamba, Saida Karoli na Jagwa Music (Tanzania) wanamuziki hawa walipendwa na karibu kila mtu,” alisema Journey Ramadhan.

Tamasha la mwaka huu lisingewezekana bila ufadhili wa Fumba Town- CPS, ambao walikuja kuokoa tamasha hili baada ya wafadhili wa awali kujiondoa kutokana na mazingira yaliyokuwa yamegubikwa na sintofahamu.

Akizungumza katika , Mkurugenzi Mtendaji wa CPS-Fumba Town, Sebastian Dietzold alisema wanajivunia kuwa sehemu ya tamasha kubwa zaidi la muziki barani Afrika ambalo kwa miaka mingi limeacha kumbukumbu za kudumu.

"Jinsi Sauti za Busara inavyoleta watu mbalimbali kutoka nchi mbalimbali kusherehekea muziki wa tamaduni mbalimbali, Fumba Town pia inawaleta pamoja watu kutoka nchi na tamaduni mbalimbali kununua na kufurahia nyumba za makazi na likizo za bei nafuu Zanzibar," alibainisha.

Tamasha la mwaka huu pia litakuwa na Movers & Shakers (jukwaa lisilo rasmi la kubadilishana uzoefu la wataalam mbalimbali), Swahili Encounters (ushirikiano wa wanamuziki wa hapa nchini na wageni), maonyesho ya Busara Plus katika Mji wa Fumba na maeneo mengine, na Tuzo ya Emerson Zanzibar Music Award, kwa wanamuziki wa hapa nchini.

Kwa taarifa zaidi: www.busaramusic.org

Tamasha la 20 la Sauti za Busara, 10 - 12 Februari 2023 linaendeshwa na Fumba Town - mradi wa CPS, Ignite Culture, CRDB Bank, Ubalozi wa Australia, Ubalozi wa Ufaransa, Institut Français, Kendwa Rocks, Adventure247 Marketing Agency, Mjini FM, ST Bongo TV, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Zanzibar Serena Hotel, Coconut FM, Zanlink, Emerson Zanzibar, 2Tech Security na zaidi.

 

Kwa marejeo:

Picha zenye ubora mkubwa, logo na vipakuzi vingine: https://www.busaramusic.org/downloads/

https://www.flickr.com/photos/sautizabusara2022/

 

 

  • This mailing list is a public mailing list - anyone may join or leave, at any time.
  • This mailing list is announce-only.

Orodha hii ya kutuma barua imekusudiwa tu kueneza habari zinazohusu Tamasha la Sauti za Busara kwa vituo au vyombo vya habari

Privacy Policy:

Sera faragha ya, Busara Promotions Press : Barua pepe zote katika orodha hii itatumika kwa madhumuni ya kukujuza shughuli zote zinazoendelea Busara Promotions. Hazitatolewa wala kupewa mtu mwingine au taasisi yeyote.