Press Kiswahili Message

 
From: "Press Kiswahili" <pressnewsletter_sw@PROTECTED>
Subject: Press Kiswahili Message
Date: February 14th 2023

Tamasha la Sauti za Busara 2023 lahitimishwa kibabe, tarehe ya tamasha la 2024 yatajwa

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Februari 14, 2023

Zanzibar. Tamasha la 20 la Sauti za Busara linalosifika kimataifa lilifikia katika kilele cha kusisimua Jumapili usiku baada ya siku tatu za burudani ya nguvu zilizoing’arisha Ngome Kongwe na vitongoji vya Mji wa Stone Town.

Tamasha la 2023 lilifanyika chini ya kauli mbiu: “Utofauti Wetu, Utajiri Wetu.” Katika maelezo yake, mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud alisema kuwa kufanyika kwa tamasha hilo ni mafanikio makubwa ikilinganishwa na namna lilivyoanza na changamoto kadhaa ilizokumbana nazo,

“Lakini, hata tulipopitia vipindi vigumu na kufikia kutaka kuachana na uendeshaji mzima wa tamasha hili, timu yetu haikukata tamaa,” alisema.

Na kupitia uhakika wa ufadhili wa taasisi ya Fumba Town ya CPS, kulipia gharama za kuendesha ofisi, uongozi wa Sauti za Busara tayari umetangaza

Kwa zaidi ya siku tatu (usiku) kulishuhudiwa burudani ya takriban vikundi 30 vikiwapagawisha watu waliohudhuria ambao walikuwa wamesafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani ili kupata mandhari ya utofauti wa muziki wa Afrika na vipaji.

Asilimia kubwa ya wale waliohudhuria, ilikuwa ni mara yao ya kwanza kwenye tamasha hilo, ambapo wengine walikuwa wamehudhuria takriban matamasha yote kwa miongo miwili, kama vile msanii maarufu Mwandale Mwanyekwa, almaarufu Mama Afrika. Wahudhuriaji wengi walionyesha kushangazwa na weledi wa hali ya juu ulioonyeshwa katika maandalizi yake, ubora wa hali ya juu wa sauti na utulivu wa burudani zote.

Wanamuziki walitoka katika kanda za Mashariki, Magharibi, Kaskazini, Kusini na Kati mwa Afrika, kwa mara ya kwanza tangu kuibuka kwa janga la Uviko-19 ambalo liliisimamisha dunia kwa miaka mitatu iliyopita.

Orodha hiyo iliyokuwa na utajiri wa vipaji ilijumuisha wasanii wa Kitanzania kama vile; Mzee wa Bwax, Damian Soul, Patricia Hillary, Zawose Reunion, Stone Town Rockerz, Uwaridi Female Band, Zan Ubuntu, Supa Kalulu, Zenji Boy na Wenzake, Waungwana Band na Culture Musical Club, Miziki ya taarab iliyoanzishwa mwaka 1958.

Pamoja na fursa za mitandao ya kubadilishana uzoefu ya 'Movers & Shakers' kwa wataalamu wa tasnia ya muziki, kipengele kingine cha tamasha la mwaka huu kilichosifiwa sana ni mradi wa 'Swahili Encounters' uliowakutanisha wanamuziki 11 kutoka Tanzania, Kenya, Zimbabwe, DRC na Sudan kwa siku nne za mazoezi na ushirikiano, na kuhitimisha na burudani ya aina yake Jumamosi usiku.

Kundi la Afrika Kusini BCUC, ambalo lilikuwa gwiji katika Sauti za Busara 2019 likiwa na jumbe zake za nguvu na maonyesho ya vilipuzi lilialikwa kurejea katika tamasha hili maalum la maadhimisho ya miaka 20, ambapo lilifanya onyesho lingine la kusisimua.

Wasanii wa kike walitoa burudani kali, ni pamoja na Asia Madani kutoka Sudan, Nasibo kutoka Zimbabwe, Naxx Bitota kutoka DRC, Atse Tewodros Project kutoka Ethiopia na Italia na Zily kutoka Mayotte sauti zao zikirindima kwenye majukwaa mawili tofauti ndani ya Ngome Kongwe.

Hata hivyo, tamasha lilipata shangwe zaidi kwa onyesho la Tiken Jah Fakoly, kutoka Ivory Coast, ambaye ni nyota mkubwa wa muziki wa reggae barani Afrika. Alitoa burudani ya nguvu ambayo ilidumu takriban saa mbili na tungo zilizojaa mashairi mazuri na ujumbe chanya, kwa Afrika na dunia.

Tamasha la 20 la Sauti za Busara liliendeshwa na Fumba Town by CPS, Ignite Culture, CRDB Bank, Ubalozi wa Australia, Ubalozi wa Ufaransa, Institut Français, Kendwa Rocks, Mjini FM, ST Bongo TV, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wakala wa Masoko wa Adventure247, Zanzibar Serena Hotel, Coconut FM, Zanlink, Emerson Zanzibar, 2Tech Security na zaidi.

Taarifa kwa mhariri: kwa ajili ya picha angavu, tembelea tovuti www.flickr.com/photos/sautizabusara2022/

na www.busaramusic.org/downloads/

  • This mailing list is a public mailing list - anyone may join or leave, at any time.
  • This mailing list is announce-only.

Orodha hii ya kutuma barua imekusudiwa tu kueneza habari zinazohusu Tamasha la Sauti za Busara kwa vituo au vyombo vya habari

Privacy Policy:

Sera faragha ya, Busara Promotions Press : Barua pepe zote katika orodha hii itatumika kwa madhumuni ya kukujuza shughuli zote zinazoendelea Busara Promotions. Hazitatolewa wala kupewa mtu mwingine au taasisi yeyote.