Sampa the Great
Country Zambia Genres hiphop fusion Website www.sampathegreat.com Facebook /sampathegreat Festival Sauti za Busara 2022 Recordings 📼The Great Mixtape, 2015; Birds And The BEE9, 2017; The Return, 2019. Sampa The Great huteremsha mashairi yenye kufikirika na kusisimua. Muziki wake una muunganiko wa ushairi, Rap na bluz huonyesha utofauti kwa vijana na kupenya mipaka yote.
Mzaliwa huyu wa Zambia aliyekulia Botswana, alianza kupata umaarufu baada ya kutoa nakala zake mbili, The Great Mixtape (2015) na Birds and the BEE9 (2017), na baadae mwaka 2019 kutoa albamu yake ya kwanza ‘The Return’.
The Return ilikuwa albamu bora ya mwaka ya Busara Promotions mwaka 2019. Albamu imesheheni ubunifu na imechanganya hiphop, neo-soul, injili, afrobeat na jazz. Ilifungua mjadala wa Uhuru, kujielezea, urithi na uhamiaji. Ni hatua ya kujitambua iliyochochewa na maisha ya Sampa nchini Australia, kifikra, kiroho na utamaduni kutoka kwa mababu zake, Zambia.
Sampa ameweza kujikusanyia mashabiki dunia nzima kutokana na maonyesho yake ya laivu. Sampa ameshafanya maonyesho kwenye matamasha mbalimbali ulimwenguni ikiwemo Glastonbury, Splendour in the Grass, Sugar Mountain, Vivid Live, Dark Mofo, Love Supreme Jazz Festival, Down the Rabbit Hole, BRIC Celebrate Brooklyn, Bushfire na mengineyo. Vilevile ameshafanya maonyesho ya ufunguzi wa wasanii wakubwa kama Burna Boy, Kendrick Lamar, Ms Lauryn Hill, Thundercat, Ibeyi na Little Simz.
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava